Serikali imeuomba uongozi Wa Agakhan kujenga hospitali nyingine kubwa katika mkoa Wa Dodoma ili kuendana na agizo la Rais Wa awamu ya tano Dkt.John Magufuli na kuboresha huduma bora za afya Mkoani humo. 
 Akizungumza hayo wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya jengo la hospitali ya Agakhan Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu amesema kuwa Agakhan wanatakiwa wajenge hospitali nyingine kubwa mkoani Dodoma ili kueneza Huduma bora za kiafya. 
 "Kutokana na Agizo la Rais Wa awamu ya tano Dkt. John Magufuli la kuhamia Dodoma inabidi na nyinyi mjenge hospitali kule" alisema Mhe. Ummy. Mhe. Ummy ameongeza kuwa kwa kujengwa hospitali hiyo Serikali itakua iokoa shilingi billion 20 mpaka 25 kwa ajili ya wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi. 
 Aidha Mhe.Ummy amesema kuwa anaushukuru uongozi Wa Agakhan kwa kuanza kujenga jengo ilo linalogharimu Billioni 112 ili kuondoa kero kwa wagonjwa Wa magonjwa yasioambukiza na kurahisiaha huduma na matibabu bora kwa wagonjwa nchini.
 Mbali na hayo Mwenyekiti wa kamati ya bodi hospitali ya Agakhan Bi. Zahra Aga Khan amesema kuwa wanampango Wa kumaliza jengo hilo kwa ajili ya kutoa Huduma bora za kiafya nchini ili kutokomeza maradhi ya mara kwa mara. 
 "Tuna morali kubwa ya kumalizia jengo hili ili tuweze kuboresha Huduma ya afya nchini kwa kutoa tiba zenye uhakika na za kisasa" alisema Bi Zahra
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa tatu kulia akitia udongo kwenye kichanja cha nondo kuashiria kuzindua rasmi ujenzi wa awamu ya pili wa jengo la hospitali ya Agakhan katika uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam, na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya bodi hospitali ya Agakhan Bi. Zahra Aga Khan.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. ni aibu kwa waziri wa afya kufurahia na kusuppport private companies zikifanya maendeleo wakati kwenye public health sector kuna uozo. vitanda havitoshi, bado wazazi wanalala chini. vijijini hakuna hata hospitali za kutosha. tuache unafiki

    ReplyDelete
  2. Ninatoa maoni haya kwa dhania kuwa habari hi in ya kweli.

    Ninadhani hapa mheshimiwa ana nia njema, yaani kuendana na agizo la Mhe. Mtukufu Rais wetu mwema.
    Jambo mmoja ambalo linaniumiza kichwa lipo katika misingi ya ubinadamu.

    Nalo jambo hilo li katika maswali machache:
    1.Kwa hiyo hospitali zilizoko Dodoma hazifai kwa matibabu ya wanadamu?,

    2. kama zinafaa, kuna mahusiano gani kati ya serikali kuhamia Dodoma na ujenzi wa hospitali kubwa ya Agha Khan??

    3. Je sio kweli kuwa binadamu wote ni sawa?

    4. Hospitali walizokuwa wakitibiwa wanaDodoma ambao ndio wengi hazifai kwa wanaSerikali wachache?

    Kwa namna yoyote IPO hali ya ubinafsi na ubaguzi, hali sote tuna thamani ileile ya UTU (Kumbuka kiapo cha wanaTANU ambacho pia ni msingi wa katiba yetu juu ya UTU na USAWA).

    Sio jambo jema viongozi kujihesabu wao kuwa tofauti na wanadamu wengine, AJIKWEZAYE ATASHUSHWA na MAJIGAMBO, KIBURI VYOTE NI DHAMBI MBELE ZA MUNGU NA WANADAMU.

    Kuiandaa Dodoma na hospitali maalumu kwaajili ya ujio wa wanasiasa ni sawa na kumaanisha:-

    ¹ Hospitali maalumu kwa afya maalum

    ² Watu waishio Dodoma sio watu maalumu na afya zao sio maalum

    ³ WanaSerikali wajao Dodoma ni watu maalum wenye AFYA maalum, UTU wenye thamani kubwa KULIKO WanaDodoma

    ⁴ Ikiwa tafsiri hizo ni sahihi, maana yake ni kuwa suala la AFYA limeingizwa katika UBAGUZI kwa kuwa kama WanaSerikali wangekuwa hawahamii Dodoma, WanaDodoma hawakustahili kuiona hospitali "KUBWA YA AGHA KHAN"

    Maoni yangu haya nimeyatoa kwa nia njema, kama yatatafsiriwa kuchafua hali ya hewa au kuumiza hisia za MTU uwe huru ndg. Bloger kuyafunga au kuyafuta, lakini nimejitahidi kwa uwezo wangu kuzingatia sana mwongozo wako. Yote kwa nia njema.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...