THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MWIGULU NCHEMBA ZIARANI MKOA WA KIGOMA

Na Abel Daud wa Globu ya Jamii, Kigoma

Waziri wa Mambo ya ndani Mh.Mwigulu Nchemba ameutaka Mkoa wa Kigoma kuendelea kukusanya silaha haramu zinazoingia nchini na kufanya shughuli za kihalifu.
Hayo ameyasema wakati akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Kigoma pamoja na maofisa mbalimbali wa Mkoani hapa katika ziara aliyoifanya hii leo ambayo inatarajiwa kumalizika hiyo kesho.
Akisoma taarifa kwa Waziri Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bw.Samson Anga,amesema mwenendo wa uingiaji wa wakimbizi Mkoania hapa si mkubwa ukilinganisha na wastani wa wakimbizi 300 kwa siku waliokuwa wakiingia hapo awali mpaka kufikia wastani wa wakimbizi 220 wanaoingia hivi sasa kwa siku.
Anga ameendelea kusema kuwa kwa sasa kuna wakimbizi wapatao 23826 mkoni hapa,hata hivyo amesema ujio wa wakimbizi Mkoani hapa umekuwa ukiathiri mazingira kwa kiasi kikubwa hasa miti imekuwa ikikatwa ovyo kwa ajili ya matumizi ya kuni katka vijiji  jirani na kambi hizo.
Waziri Nchemba amesema taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ambaye ni Mkuu wa Wilayaa ya Kigoma Bw.Samson Anga jitihada zinazoendelea
kufanyika kukamata siraha haramu zinapaswa kuendelea kwa kuwa madhara yaletwayo na siraha hizo ni makubwa mno.

 Waziri Chemba akilakiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na baadhi ya maofisa
 Mh.Nchemba akisalimiana na Mkuu wa Takukuru mkoani Kigoma
 Maafisa wa polisi wakimsikiliza Waziri Nchemba
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kgoma Bw.Samson Anga akisoma taarifa fupi
Mhe. Nchemba Akizungumza na Kamati ya ulinzi na usala pamoja na maofisa wa serikali wa mkoa