Baadhi ya Wananchi wakijaza Fomu ya Kujiunga na WOTE SCHEME katika Banda la PPF Viwanja vya Nane Nane Ngongo Kama Picha Inavyoonekana Afisa Uhusiano Mwandamizi, Janet Ezekiel akitoa maelekezo ya Jinsi ya Kujaza Fomu Hizo.
Wananchi waliotembelea Banda la PPF, wakimsikiliza kwa Makini Afisa Masoko PPF Wakati akitoa Elimu Juu ya Mfumo wa WOTE SCHEME.
Baadhi ya Wananchi wakijaza Fomu ya Kujiunga na WOTE SCHEME katika Banda la PPF Viwanja vya Nane Nane Ngongo Kama Picha Inavyoonekana Afisa Uhusiano Mwandamizi, Janet Ezekiel na Afisa Masoko PPF, Wakitoa maelekezo ya Jinsi ya Kujaza Fomu Hizo.
Afisa Uhusiano Mwandamizi, Janet Ezekiel akimkabidhi kadi ya WOTE SCHEME kwa mwananchi aliyejiunga na Mfuko huo.

Mfuko wa Pensheni wa PPF upo katika Viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi katika Maonesho ya Nane nane ili Kutoa Elimu kwa Wananchi juu ya Mfumo wa WOTE SCHEME kwa Sekta Binafsi kama Vile Wakulima,Wafugaji, Mama Lishe, Madereva Bodaboda na Wajasilamali mbalimbali ili waweze kujiwekea Akiba wakati huohuo wakinufaika na Bima ya Afya, Mikopo kwa Ajili ya Kujiendeleza Kielimu, Kuongeza Mtaji na Kunufaika na Pensheni za kila Mwezi.

Akiongea, Bi Janeth ametoa wito kwa wadau mbalimbali kutembelea Banda hilo la PPF kwa ajili kupata elimu na kujiunga na mfuko huo na kufaidika na fursa zinazotolewa na PPF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...