THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

yale yaleeeee... vijipu upele mbagala rangitatu jijini Dar es salaam

 Wazee wa kijiweni katika eneo la Mbagala Rangi tatu jijini Dar es salaam wakipata kikombe cha kahawa huku pembezoni kukiwa na lundo la uchafu lililotolewa kwenye mtalo kama alivyokutwa na kamera ya Globu ya Jamii
 Mdau wa Mbagala akiwa katika harakati  za kutafuta chupa kwa ajili ya biashara. Watu mbalimbali wamejiajili wenyewe kwa kufanya biashara za kuuza chupa tupu.
 Mfanyakazi wa usafi  akitimiza wajibu wake katika harakati za kuliweka jiji safi  katika eneo la Mbagala rangi tatu jijini Dar es Salaam leo.
Mama lishe akipika chapati kwa ajili ya wateja wake jirani na rundo la taka katika eneo la Mbagala rangi tatu wilayani Temeke jijijni Dar es Salaam leo.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii


Kuna Maoni 3 mpaka sasa.

 1. Nasra Mohammed Anasema:

  Halafu anakula mchuzi ni harufu kutoka kwenye lundo la taka. Aibu yetu Watanzania!

 2. Anonymous Anasema:

  Hii inavyotkea hivi ni janga la Taifa. Serikali inatumia millioni za fedha itokeapo magonjwa ya miripuko. Binadamu wanakosa afya na maendeleo yao yanadumazwa kutokana na magonjwa mbali mbali yatokanayo na kuishi na uchafu kama hivyo.

  Kuna watu wenyekazi zao ambazo ni kuelimisha jamii kuhusu athari za uchafu na isivyo sahihi kuishi nao katika maisha ya kila siku. Kuna viongozi wa Serikali za mitaa na vitongoji tuishivyo. Pia kuna viongozi wateule kabisa wanaotambulika kwenye usimamizi wa afya na usafikatika haya maeneo tuishiyo. Hawa wotehawa ina maana hawayaoni haya aundo wanafanya kusudi eti kwa kutaka viongozi wakuu wa nchi au Mkoa waje kutolea ukali. Na haohao niliowataja wanaohusika na uondoshwaji na kutoa elimu kwa umma huwa mbelembele kupiga teke biashara za wananchi pale waonapo viongozi wa ngazi za juu wanatembelea sehemu zao. Sasa kama hao viongozi wa maeneo yetu tuishiyo wangekuwa makini hakungekuwepo na kitu cha kukipiga teke wakati viongozi wanatembelea.

  Wananchi wanahitaji kuelimishwa kuhusu maisha yao na usafi, pia usafi wa mazingira na kujiepusha na magonjwa mbalimbali yakiwemo yale ya mlipuko. Wale wahusikao na kazihizi hebu tusaididenisisi wananchi kutueleimisha na kutuelekeza kuhusu haya. Nasi tunaona vibaya wakati mwingine kuishi na huu uchafu na pia tunaumia tuonapo wale tuwapendao na wanafamilia wanaugua. Mamlaka za kuzoa na kusafisha taka fanyeni kazi zenu na mtuhudumie kwani sisi tunaotakiwa kulipa mbona tunalipa stahiki na staili zote kwenye Mamlaka husika. K

  Kama itatokea viongozi wa juu wanaona makala hii, tafadhalini tusaidieni kuwashtua hao wahusika katika makazi yetu wafanze stahiki zao kwetu

 3. Anonymous Anasema:

  hata vijijini kumekuwa kuchafu siku hizi.