Wazee wa kijiweni katika eneo la Mbagala Rangi tatu jijini Dar es salaam wakipata kikombe cha kahawa huku pembezoni kukiwa na lundo la uchafu lililotolewa kwenye mtalo kama alivyokutwa na kamera ya Globu ya Jamii
 Mdau wa Mbagala akiwa katika harakati  za kutafuta chupa kwa ajili ya biashara. Watu mbalimbali wamejiajili wenyewe kwa kufanya biashara za kuuza chupa tupu.
 Mfanyakazi wa usafi  akitimiza wajibu wake katika harakati za kuliweka jiji safi  katika eneo la Mbagala rangi tatu jijini Dar es Salaam leo.
Mama lishe akipika chapati kwa ajili ya wateja wake jirani na rundo la taka katika eneo la Mbagala rangi tatu wilayani Temeke jijijni Dar es Salaam leo.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Halafu anakula mchuzi ni harufu kutoka kwenye lundo la taka. Aibu yetu Watanzania!

    ReplyDelete
  2. Hii inavyotkea hivi ni janga la Taifa. Serikali inatumia millioni za fedha itokeapo magonjwa ya miripuko. Binadamu wanakosa afya na maendeleo yao yanadumazwa kutokana na magonjwa mbali mbali yatokanayo na kuishi na uchafu kama hivyo.

    Kuna watu wenyekazi zao ambazo ni kuelimisha jamii kuhusu athari za uchafu na isivyo sahihi kuishi nao katika maisha ya kila siku. Kuna viongozi wa Serikali za mitaa na vitongoji tuishivyo. Pia kuna viongozi wateule kabisa wanaotambulika kwenye usimamizi wa afya na usafikatika haya maeneo tuishiyo. Hawa wotehawa ina maana hawayaoni haya aundo wanafanya kusudi eti kwa kutaka viongozi wakuu wa nchi au Mkoa waje kutolea ukali. Na haohao niliowataja wanaohusika na uondoshwaji na kutoa elimu kwa umma huwa mbelembele kupiga teke biashara za wananchi pale waonapo viongozi wa ngazi za juu wanatembelea sehemu zao. Sasa kama hao viongozi wa maeneo yetu tuishiyo wangekuwa makini hakungekuwepo na kitu cha kukipiga teke wakati viongozi wanatembelea.

    Wananchi wanahitaji kuelimishwa kuhusu maisha yao na usafi, pia usafi wa mazingira na kujiepusha na magonjwa mbalimbali yakiwemo yale ya mlipuko. Wale wahusikao na kazihizi hebu tusaididenisisi wananchi kutueleimisha na kutuelekeza kuhusu haya. Nasi tunaona vibaya wakati mwingine kuishi na huu uchafu na pia tunaumia tuonapo wale tuwapendao na wanafamilia wanaugua. Mamlaka za kuzoa na kusafisha taka fanyeni kazi zenu na mtuhudumie kwani sisi tunaotakiwa kulipa mbona tunalipa stahiki na staili zote kwenye Mamlaka husika. K

    Kama itatokea viongozi wa juu wanaona makala hii, tafadhalini tusaidieni kuwashtua hao wahusika katika makazi yetu wafanze stahiki zao kwetu

    ReplyDelete
  3. hata vijijini kumekuwa kuchafu siku hizi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...