THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

YANGA, AFRICAN LYON WAKAMILISHA USAJILI KWA TMS.

Afisa habari wa TFF Alfred Lucas.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Nchini TFF, limethibisha kukamilika kwa usajili wa timu 11 zilizokuwa hazijakamilisha usajili wake kwa mfumo wa TMS baada ya kuongezewa muda wa masaa 48 baada ya kufungwa kwa dirisha la awali.

Akizungumza na Michuzi Globu, Afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema kuwa timu zote  11 zimeshakamilisha usajili wake kwa njia ya TMS baada ya kuongezewa muda wa masaa 48 na shirikisho la mpira wa Miguu Duniani FIFA.

Awali dirisha la usajili nchini lilifungwa Agosti 06 huku timu kadhaa ikiwemo Yanga na  African Lyon za ligi kuu zikiwa hazijafanya usajili wake n kutakiwa kuandika barua za utetezi ili kuweza kupata fursa ya kufunguliwa tena kwa dirisha la usajili.

Lucas amesem kuwa, baada ya kutum utetezi wao uliwasilishwa FIFA na wakapewa masaa 48 kukamilisha usajili huo huku TFF wakizipiga faini timu za ligi kuu kwa kulipa kiasi cha milioni tatu na timu za ligi daraja la kwanza wakitakiwa kulipa milioni moja.

Kumalizika kwa usajili huo timu kwa sasa zinaweza kuendelea na taratibu za kujiandaa na ligi huku wakisubiri mapingamizi kwa wachezaji waliowasajili.