TIMU ya Yanga yenye makao yake Mtaa wa Twiga na Jangwani imefanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza katika Mashindano ya Kombe la Shirikisho, baada ya kupata goli 1-0 lililofungwa na Mchezaji wa kimataifa kutoka nchini Burundi, Amisi Tambwe dakika ya tatu ya mchezo dhidi ya Timu ya Mo Bejaia ya nchini Algeria, mechi iliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.
Akizungumza baada ya kupata ushindi huo, Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Van De Pluijm amesema ushindi huu umempa nguvu katika kuelekea mchezo unaofuata dhidi ya TP Mazembe.
Pluijm amesema kuwa, wachezaji wake wamecheza vizuri sana na wameweza kulinda goli katika dakika zote ingawa kuna makosa madogo madogo yaliyojitokeza ila anawapa hongera kwa jitihada walizozifanya. 
 Naye Nahondha wa Yanga, Vicent Bossou amesema wamefanya kazi kubwa sana katika kuhakikisha wanatoka ushindi na wamecheza timu nzuri sana yenye uzoefu wa muda mrefu wa michuano ya kimataifa ila anawapongeza pia wachezaji wenzake kwa jitihada walizozifanya.
Baada ya ushindi huo Yanga wanaendea kusalia katika nafasi ya nne wakiwa na alama nne huku mchezo kati ya Mazembe na Medeama ukitarajiw kuchezwa kesho nchini Ghana. 
 Mshambuliaji wa Yanga, Obren Chirwa akiwa katikati ya Mabeki wa Timu ya Mo Bejaia.
 Washabiki wa Timu ya Yanga wakiishangilia timu yao baada ya kupata ushingi dhidi ya Timu ya Mo Bejaia ya Algeria, katika Mechi ya Kombe la Shirikisho iliyopigwa jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda Bao 1-0.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...