Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KUELEKEA Mkutano Mkuu wa wanachama wa Yanga ulioitishwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji , Uongozi wa Yanga kupitia kwa mratibu wa Matawi na Mkuu wa Kitengo cha Masoko Omary Kaya  amezitaja ajenda kuu zitakazotumika kwenye mkutano huo huku suala la Mabadiliko ya Katiba ya Yanga yakipewa kipaumbele. Katika mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kesho siku ya Jumamosi unatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya wanachama wanaotaka kufahamu mwenendi mzima wa timu ya yao.

Amesema katika mkutano huo ajenda zitakazojadiliwa ni ushiriki wa timu yao katika michuano ya kimataifa ikiwemo hatua waliyofika katika mashindano ya Kombe la Shirikisho, pili suala linguine ni  ushirikiano mdogo wanaoupata kutoka ndani ya Shirikisho la Soka Nchini(TFF) na kipi kifanyike ili kukuza uhusino mzuri na shirikisho hilo huku ajenda ya tatu ikibeba katiba ya klabu pamoja na maboresho yanayotakiwa kufanyika ili kupata katiba bora.

Mapato na matumizi yatakuwa katika ajenda namba tano pamoja na kuto shukrani kwa uongozi uliopita kwa kazi kubwa waliyoifanya na kukaribisha uongozi mpya. Kingine ni maendeleo ya klabu hiyo pamoja na kuangalia mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu yao ili kuhakikisha inapata maendeleo zaidi ya yaliyofanyika kipindi cha nyuma na endapo wanachama watakubaliana na jambo hilo litaanza utekelezaji haraka.

"Endapo tutakubalia kuingia katika mfumo wa kampuni basi tutaami huko na wanachama wanatakiwa kielewa kuwa hatujakurupuka katika jambo hili bali tumefanya utafiti wa kutosha" amesema Kaya. Wanachama wanatakiwa kuhudhuria kwa wingi ili kuleta maendeleo na mabadiliko ya pamoja ndani ya klabu hiyo kongwe hapa nchini. Baada ya kumalizika kwa mkutano huo Yanga itashuka dimbani kuvaana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa kirafiki utakaochezwa ndani ya uwanja wa Taifa na kiingilio cha mchezo huo kitakuwa 5,000 huku pia mchezo huo ukiwa sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wao wa marudiano dhidi ya Mo Bejaia.

Mabingwa hao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara  msimu uliopita, timu ya Yanga imegoma kutumia jezi mpya zilizotolewa na mdhamini mkuu wa ligi hiyo juzi. Kaya amesema kuwa jezi yake ya ugenini inafanana na ile waliyotumia msimu uliopita hivyo hawatapata faida katika mauzo ya jezi hizo.

Pia wamesema kuwa hawakushirikishwa katika mchakato wa kuandaa jezi hizo ambazo zimetengenezwa kwa kiwango cha chini sana. Yanga haina hadhi ya kuvaa jezi zisizo na bora na kiwango kisichoridhisha kama kilichotumika kutengenezeanjezi hizo.   "Sisi ni klabu na tunajiendesh kibiashara tutauza vipi jezi zetu na kupata faida kama zinafanana na zile za mwaka jana pia timu yetu haiwezi kuvaa jezi zisizo na ubora kama hizi zilizotolewa na wadhamini wetu", amesema Kaya.

Amesema kikubwa watakachokifanya ni kuhakikisha wanafuata na kuheshimu nembo ya mdhanimi katika jezi watakazotumia msimu ujao wa ligi kuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...