Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (katikati),Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Kandanda nchini, Salum Madadi (kulia), Mwenyekiti wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania, Amina Karuma (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isaack Nchunda (kushoto) na nahodha wa timu ya Kilimanjaro QueensSophia Mwasikili wakilishikilia kombe la mabingwa wa Challenge Afrika Mashariki na Kati 2016 lililotwaliwa na Kili Queens, wakati timu hiyo ilipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam .
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso  na nahodha wa timu ya Kilimanjaro QueensSophia Mwasikili wakilishikilia kombe la mabingwa wa Challenge Afrika Mashariki na Kati 2016 lililotwaliwa na Kili Queens, wakati timu hiyo ilipotembelea ofisi za Airtel
 Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya akiongea na timu ya Kilimanjaro Queens na waandishi wa habari  wakati  timu  hiyo ilipotembelea makao makuu ya kampuni ya Airtel  jijini Dar es Salaam . Asilimia kubwa ya wachezaji wa Kili Queens ni matunda ya mashindano ya Airtel Rising Star.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso  akiongea na timu ya Kilimanjaro Queens na waandishi wa habari  wakati  timu  hiyo ilipotembelea makao makuu ya kampuni ya Airtel  jijini Dar es Salaam. wakishuhudia ni  Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Kandanda nchini, Salum Madadi (katikati) akifatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isaack Nchunda
Timu ya wanawake Tanzania ya Kilimanjaro Queens ikiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Airtel na TFF wakati timu hiyo ilipotembelea ofisi za Airtel leo. Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Safi sana Airtel ,msiishie kufadhili tu kwenye Airtel Rising Star bali pia muifadhili ligi ya wanawake ambayo ni changa na inaitaji kukua ,kwa kufanya hivyo itasaidia kuendeleza vipaji vilivyoibuliwa kwenye program ya Airtel Rising Star na kuhakikisha nafasi nzuri zaidi ki rank kwa soka ya wanawake lakini pia kuwatangaza nyie Airtel kama kampuni yenye mafanikio kwenye program zake za Michezo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...