THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

SAUTI SOL WAACHIA VIDEO YA ‘KULIKO JANA’

Majagina wa muziki wa Afrika Mashariki na washindi wa tuzo kibao, Sauti Sol (Kenya) wameachia video ya wimbo wao unaofanya vizuri, KULIKO JANA, uliopo kwenye santuri yao ya tatu: Live and Die in Afrika. Bien wa Sauti Sol anaelezea maana ya wimbo huo, “Unamaanisha kuwa uaminifu wa Mungu haukomi kamwe. Huruma yake haiishi – kila uchao ni vipya.” Wakimshirikisha Redfourth Chorus (Upper Hill School), wimbo huo mtamu lakini wenye ujumbe mzito, umezikwea chati na kuwagusa mashabiki barani Afrika na zaidi.

Video maarufu ya Sauti Sol wakiimba akapela ya wimbo huo wakiwa na Redfourth Chorus, ulivutia masikio ya watu mashuhuri duniani na kwenye vyombo vya habari hadi kumfanya Amber Riley, nyota wa kipindi kilichoshinda tuzo za Emmy, Glee, kuandika kwenye Instagram, “Sielewi wanachokisema lakini najua ni kizuri. Inasikika kimalaika, kuna yeyote anayejua kama kuna video?” Mastaa wengine waliowahi kuiweka video hiyo kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja Master P, Anthony Hamilton, Jb Smoove na  WorldstarHipHop, miongoni mwa tovuti zingine za habari za kimataifa.

Katika video mpya iliyotoka yenye rangi nyeusi na nyeupe ya KULIKO JANA, Sauti Sol wameungana na chipukizi lakini mweye kipawa cha hali ya juu, Redfourth Chorus kwa maajabu ya kimuziki. Sauti Sol wamesema kwenye taarifa yao, “KULIKO JANA ni wimbo maalum sana kwetu. Ulihamasishwa na safari yetu na rehema zisizoisha, mapenzi na baraka ambazo Mungu ametuonesha muda wote licha ya udhaifu wetu.”

Video ya KULIKO JANA imetayarishwa na Fulfillment Limited, na kufanyika Kenya na waongozaji wakiwa Tim Mwaura na Joash Omondi.  Wimbo umeandikwa na kutayarishwa na Sauti Sol.  Kipande cha akapela kilipangwa na Philip Tuju na Redfourth Chorus.