Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Wilson Masilingi akiongea na Watanzania wa North Carolina siku ya Jumamosi Septemba 3, 2016 katika ukumbi wa hoteli ya Comfort Suites jijini Durham, North Carolina. Katika hotuba ya Mhe. Balozi Wilson Masilingi aliwaasa wanaUTNC kupendana na kushikamana na kusaidiana kuonyeshana njia za mafanikio badala ya kukalia majungu na kuchukia maendeleo ya mwenzako. Mwenzako anapofanya vizuri mpe sifa yake na muulize amefikaje hapo na yeye akusaidie ufikie hapo alipo.

Mhe. Balozi Wilson Masilingi aliwasisitizia Watanzania wa North Carolina wajenge desturi ya kuwekeza nyumbani na kuwaelekeza jinsi ya kufungua akanti za akiba kwenye benki za Tanzania ili ziweze kuwasaidia kwa siku za usoni kwa maendeleo yao nchi Tanzania kwa kuwezesha kununua kiwanja na hatimae kujijengea kibanda.

Mhe. Wilson Masilingi aliwasisitizia wanajumuiya hao kutafuta wawekezaji watakaoingia nao ubia na wahakikishe hawaingii mikataba na watu wa kati na yeye kwa kutumia ofisi ya Ubalozi ameahidi kuwasaidia ili kuwaondolea wawekezaji usumbufu unaoweza kujitokeza pindi wanapoamua kujifanyia wenyewe kwani wanaweza kuangukia kwenye mikono isioitakia mema Tanzania.

Mhe. Balozi aliwaachia uongozi wa Jumuiya hiyo ya Umoja wa Watanzania North Carolina wito wa kuunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli za kuchangia madawati na Mwenyekiti mstaafu awamu ya tatu, Bwn. Geofrey Lepana aliitikia wito huo kwa kuchanga dola 80 pesa taslimu papo hapo kwa Mhe. Balozi Wilson Masilingi na yeye kuukabidhi mchango huo kwa mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa Watanzania North Carolina, Bi. Gloria Alex na yeye kuahidi kwa niaba ya uongozi wake kuufanyia kazi wito huo.
Afisa Ubalozi Bwn. Abbas Missana akifuatilia hotuba ya Mhe. Balozi Wilson Masilingi.
Bwn. Nassoro Basalama, mwenyekiti mstaafu akidadavua historia ya jumuiya hiyo kwa Mhe. Balozi Wilson Masilingi.
 Mwenyekiti mstaafu Geofrey Lepana akipena mikono na Mhe. Balozi Wilson Masilingi mara baada ya kuchangia dola 80 kwa ajili ya madawati.
Mhe. Balozi Wilson Masilingi akimkabidhi mchango huo mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania North Carolina, Bi. Gloria Alex.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...