Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Bw Godfrey L. Mngereza akizungumza katika kikao cha Mahusiano mema kati ya BASATA na Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Mkurugeni wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure na Mratibu wa Program ya Museum Art Explosion Bw Edgar Chatanda wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa BASATA Bw Godfrey L. Mngereza (hayupo pichani)

Na SIXMUND J. BEGASHE - Makumbusho ya Taifa.

Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni imekutana na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na kufanya mazungumzo ya namna vyombo hivi viwili vya Serikali vitakavyo weza kudumisha mashirikiano katika shughuli za kila siku ili kuhifadhi na kuendeleza Sanaa na Utamaduni wa Mtanzania.

Akizungumza kwenye kikao hicho Katibu Mtendaji wa BASATA Bw Godfrey L. Mngereza ameipongeza Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kwa kuanzisha Program ya kila mwisho wa mwezi “Museum Art Explosion” ili kutoa nafasi kwa wasanii wa Tanzania kuosesha kazi zao za sanaa za Ufundi na za jukwaani kitu ambacho kinasaidia kukuza pato la msanii na pia kuutangaza Utamaduni wetu.

“Mashirikiano yetu BASATA na Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam yatasaidia vyombo hivi hasa Makumbusho kufanya kazi za Sanaa na Utabaduni kwa usalama mkubwa kwa kuwa BASATA itasaidia kuwamulika wasanii wasio tambuliwa na Baraza ambao watataka kufanya maonesho kwenye Makumbusho yetu na hasa kwenye hii program ya Museum Art Explosion” Aliongeza Bw Mngereza.

Nae Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure, ameeleza kuwa mahusiano ya BASATA na Makumbusho hiyo ni ya kihistoria kwani BASATA ilihusika kwa kiasi kikubwa kwenye kutoa ushauri juu ujenzi wa mradi wa Nyumba ya Utamaduni na namna itakavyo tekeleza kazi zake za Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni Nchini.

“Japokuwa tunatekeleza kazi zetu za msingi kama Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kwa kupitia program mbali mbali za sanaa na Utamaduni lakini tumeona ni vyema tukakutana na wenzetu wa BASATA ili watuongezee maarifa zaidi ya namna ya kuziboresha hizi program zetu hususani hii ya MUSEUM ART EXPLOSION maana wao ni wabobezi wa Sanaa na Utamaduni”. Alisema Bw Bufure

Kikao hicho kilicho udhuriwa na wajumbe wa tano kutoka Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni na wanne kutoka BASATA kiliangazia mashirikiano katika nyaja ya Utoaji elimu kwa Wasanii, Mawasiliano, Utafiti na Maonesho ya kazi za Sanaa hivyo kamati ndogo ziliundwa ili zitoke na mapendekezo zaidi yatakayo wezesha vikao vya juu kupitia na kupitisha maamudhi sahii. Na SIXMUND J. BEGASHE Wa Makumbusho ya Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...