Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya TIB Corporate Bw Frank Nyabundege (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi y ash milioni 10 kwa Mkurugenzi wa taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) Dk. Julius Mwaiselage (kulia) kuiwezesha taasisi hiyo kukabiliana na mahitaji mbalimbali katika matibabu ya wagonjwa wa saratani wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw Charles Singili (wa pili kushoto).
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw Charles Singili (kushoto) akizungumza wakati wa hafla hiyo.
 
Benki ya TIB Corporate imetoa msaada wa sh mil 10/- kwa taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) ikilenga kuiwezesha taasisi hiyo kukabiliana na mahitaji mbalimbali katika matibabu ya wagonjwa wa saratani.Msaada huo ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo katika kuisaidia jamii kupitia mpango wake wa Uwajibikaji kwa jamii.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mteandaji wa benki hiyo Bw Frank Nyabundege alisema taasisi hiyo ina uhuru wa kuchagua mahali inapoweza kuelekeza matumizi ya pesa hizo kulingana na vipaumbele vyake.

“Tunaunga mkono jitihada zinazofanywa na ORCI katika kukabiliana na saratani hapa nchini na ndio maana na sisi tukaona tuna wajibu wa kuunga mkono jitihada hizo kwa kuchangia kiasi hiki cha pesa ili kisaidie kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili taasisi hii muhimu zikiwemo,’’ alibainisha Bw Nyabundege.

Alisema uwepo wa taasisi hiyo ni fahari kwa taifa kwa kuwa imekuwa ikisaidi mapambano dhidi nya ugonjwa huo ambao umekuwa kikwazo katika uzalishaji kwa kuwa umekuwa ukishambulia nguvu kazi ya taifa.

“Matibabu ya ugonjwa huu pia yamekuwa yakihusisha gharama kubwa na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya kiuchumi katika ngazi za kifamilia,’’ aliongeza.Alitoa wito kwa watu binafsi na mashirika mengine kujitokeza na kusaidia taasisi hiyo ya Serikali kwa kiasi chochote.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi wa taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage alisema kwa sasa taasisi yake inakabiliwa na ongezeko la wagonjwa huku akikabiliwa na uhaba wa miundombinu na dawa na vifaa tiba vinavyoendana na ongezeko hilo na hivyo kutoa wito kwa mashirika, taasisi na watu binafsi kuisaidia taasisi hiyo.

“Kwa takwimu za mwaka jana tulipokea wagonjwa zaidi ya elfu tano ikilinganishwa na wagonjwa 1500 kwa mwaka tuliokuwa tukiwapokea miaka ya nyuma wakati taasisi inaanza,’’ alisema huku akitaja baadhi ya sababu za ongezeko la ugonjwa kuwa ni pamoja na aina ya vyakula vinavyoliwa na kwa sasa, matumzi ya tumbaku na ukosefu wa mazoezi miongoni mwa wana jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...