THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

CDF TROPHY YAANZA KWA KASI LUGALO GOLF CLUB

Selemani Semunyu JWTZ

Kombe la Mkuu wa Majeshi kwa Mchezo wa Golf CDF Troph imeanza kwa Michezo ya awali ambapo  Wapiga mikwaju wa kulipwa wamechuana vikali huku Geofrey Reverian  na Klabu Lugalo na Farai Chitengwa  wa Zimbambwe wakilazimika kurudia mchezo baada ya kufungana.

Katika mashindano hayo yanayofanyika katika Uwanja wa Lugalo Golf Club Jijini Dar es salaam wamefungana  mikwaju ya jumla (gross) 72 kwa kila mmoja na kulazimika kutakiwa kurudia mchezo kwa kucheza viwanja vitatu hali itakayoamua nani kuibuka mshindi katika kundi la wapiga mikwaju wa kulipwa.

Katika nafasi ya tatu ya Wapiga Mikwaju hao wa  kulipwa imechukuliwa na Salim Mwenyenza aliepata mikwaju ya Jumla 74 ikiwa ni kati ya wachezaji wa kulipwa 20 walioshiriki katika kinyanganyiro hicho ambacho mshindi atajulikana jumamosi Septemba 23 mwaka huu.

Katika hatua Nyingine wacheza Golf wa kundi la Wachezaji Wasaidizi (Carde) 30 walipambana kupata mbabe wa kundi hilo ambapo Richard Mtweve aliibuka na ushindi kwa kupata Net 69 baada kupigaMikwaju ya Jumla 76  huku akicheza kwa kiwango cha Saba.

Nafasi ya  pili imechukuliwa na Rasuri Shaban baada ya kupata Net 70 baada ya kupiga mikwaju ya Jumla 79 huku kiwango cha Uchezaji kikiwa ni Tisa na Mwanamke pekee kwa kundi hilo Rose Nyenza kushika Nafasi ya tatu baada ya kupata net ya 87 baada ya kupiga mikwaju ya Jumla 111 na kiwango cha Uchezaji kikiwa ni 24.

Michezo hiyo ya Kombe la Mkuu wa  majeshi ya Ulinzi CDF Trophy yanatarajiwa kuendelea na kufikia tamati Jumamosi Septemba 24 katika Uwanja wa Golf wa Lugalo ambapo wachezi wa makundi matatu watachuana.

Makundi hayo ni Senior,Junior, Ladies na  Daraja la A Daraja B na daraja C  ambapo mbapo pia mshindi wa Jumla atapatikana kutoka katika Makundi hayo.

Mgeni Rasmi katika Mashindano hayo ya Kombe la Mkuu wa majeshi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda.
Mwenyekiti wa Klabu ya golf ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo (Katikati) akiangalia mazoezi ya wachezaji wa Klabu hiyo wanaotaraji kushuka Uwanjani kuwania CDF Trophy.
Mkuu wa majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara akikata utepe kuzindua Daraja la Kiwanja namba Tisa cha Golf Lugalo ikiwa ni sehemu ya kuboresha uwanja huo na kuwa na sifa zaidi kwa mashindano mbalimbali yakiwemo ya Kimataifa. (Picha na Luteni Selemani Semunyu).