THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

CHAMA CHA WAFUGAJI NCHINI CHATOA TAMKO KUFUATIA CHANGAMOTOKUBWA ZINAZOWAKABILI

Mkuu wa Chama cha Wafugaji Tanzania (pichani kati),Magembe Makoye akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar kuhusiana na mambo mbalimbali yanayowakabili wafugaji hapa nchini,kushoto ni Mfugaji kutoka Suwambawaga,Mayunga Gamas na kulia ni Charles Mtokambati.

Bwa.Maghembe Makoye alieleza changamoto mbalimbali zinazowakabili wafugaji hao kuwa ni Ukosefu wa Maeneo rasmi ya malisho,Migogoro Baina ya Wakulima na Wafugaji,Migogoro kati ya Wafugaji na Idara ya Maliasili na Wanyamapori.Akaeleza kuwa kwa sasa kuna Mgogoro mkubwa kati ya Idara za Maliasili na Wanyamapori ndani ya Wizara ya maliasili na utalii na Wafugaji,akafafanua kuwa changamoto hizo zimekuwa sugu kutokana na kupanuka kwa maeneo ya Maliasili na kuchukua maeneo ya Wafugaji.

"Wafugaji wamekua wakifukuzwa kutoka kwenye maeneo hayo ambayo hapo awali walikuwa wakiyatumia kwa malisho,baada ya kuchukuliwa na maliasili na kuwa sehemu ya maeneo yaliyohifadhiwa.
Mkuu wa Chama cha Wafugaji Tanzania (pichani kati),Magembe Makoye akionesha baadhi ya Nyaraka kwa waandishi wa habari,zinazoeleza kukamatwa kwa ng'ombe za wafugaji hao zaidi ya elfu moja na Wizara ya Maliasili na Utalii,ambapo mahakama iliamua kuwa Maliasili na Utalii irejeshe Ng'ombe hao kwa wafugaji,ambapo mpaka sasa kwa mujibu wa taarifa ya wafugaji hao hakuna kilichofanyika mpaka sasaKuna Maoni 2 mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    ...makao makuu ya chama yapo Dar es Salaam. Kuna wafugaji Dar es Salaam kweli?

  2. Anonymous Anasema:

    Bodi ya pamba - Dar
    Stamico - Dar
    Bodi ya korosho - Dar