Mkuu wa wilaya ya Handeni, Mh. Godwin Gondwe ametembelea kambi tiba ya GSM Foundation yenye lingo la kuokoa watoto zaidi ya 3500 wanaodaiwa  kupoteza maisha kila mwaka kutokana na kuzaliwa na tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi.
 
Inasemekana zaidi ya Watoto 4000 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi huzaliwa kila mwaka nchini na wanaoripotiwa hospitalini si zaidi ya 500 hatua ambayo imechangia kwa asilimia kubwa ongezeko la watoto wenye mtindio wa ubongo huku baadhi yao wakipoteza maisha kwa sababu ya kukosa Tiba.

Akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga "Bombo" wakati wa zoezi la Upasuaji wa watoto hao lilipokuwa likiendeshwa na madaktari Bingwa, Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji ya (MOI)iliyopo Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili, Dkt Othman Kiloloma alisema ongezeko la watoto hao linatokana na ukosefu wa lishe yenye virutubisho vijulikanavyo kwa jina la “Folic Acid”

Alisema kukosekana kwa lishe hiyo kumesababisha tatizo hilo kwa watoto ambalo lisipopatiwa ufumbuzi wa kina linaweza kupelekea athari kubwa kwao ikiwemo vifo hali inayoweza kupunguza jamii ambayo ingeweza kuchangia ukuaji wa uchumi katika shughuli za uzalishaji.

“Ukiangalia kwa hivi sasa zaidi ya watoto wapato 4000 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi huzaliwa kila mwaka nchini na wanaoripotiwa hospitalini si zaidi ya 500 hatua ambayo imechangia kwa asilimia kubwa ongezeko la watoto wenye mtindio wa ubongo huku baadhi yao wakipoteza maisha kwa sababu ya kukosa hivyo jamii inapaswa inapaswa kuwapeleka katika Hospitali ili kuweza kuchangia ukuaji wao na maendeleo “Alisema

Akizungumzia kuhusu changamoto zinazosababisha watoto hao kukosa huduma za upasuaji, Afisa Habari wa Taasisi ya Afya inayojihusisha na Upasuaji wa watoto hao, Khalfani Kiwamba alisema kuwa upungufu wa madaktari wenye taaluma ya upasuaji wa waathirika hao ni mkubwa kwa sababu nchini wapo saba ambapo sita wapo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na mmoja yupo hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Bugando.

Awali akizungumza katika zoezi hilo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Godwin Gondwe aliipongeza taasisi inayojihusisha kusaidia sekta ya Afya na Elimu hapa nchini (GSM) kwa kutoa matibabu ya upasuaji huo kwa watoto hali ambayo itawasaidia kuweza kurejea kwenye hali zao za kawaida.

Alisema katika suala kama hilo jamii haina budi kuacha kuwaficha watoto wenye matatizo hayo badala yake waona namna ya kuwasiliana na viongozi wao ngazi za chini kuwaepusha na vifo ambavyo vinaweza kuwakumba kutokana na hali walizonazo.
 
“Lakini pia lazima jamii ibadilike kuona umuhimu wa kuacha kuwaficha watoto wenye matatizo hayo badala yake wawapeleke kwenye hospitali zilizopo karibu nao kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambayo yatawasaidia kupona “Alisema.

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam Dkt Othumani Kiloloma kulia akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Godwin Gondwe kushoto ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni alipotembelea Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kunapofanyika zoezi la upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi lililofanywa na Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Dkt Karia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...