THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

DC KIGAMBONI APEWA SIKU MBILI KUHAKIKISHA FUKWE ZOTE ZA KIGAMBONI ZIKO SAFI

 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga  Mpina amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bw. Hashim Mgandilwa kuhakikisha fukwe zote za kigamboni zinafanyiwa usafi na kuwa katika hali ya kuridhisha.

Naibu Waziri Mpima ameseyasema hayo leo katika maeneo ya fukwe za kigamboni aliposhiriki katika siku ya  usafi kitaifa ya mwezi wa September.
Amesema fukwe za kigamboni ni chafu sana na usafi wa mazingira katika mji wa kigamboni hauridhishi, “pamoja na wananchi kujitokeza kwa wingi katika kusafisha mazingira leo fukwe ni chafu na wengine wanatuangalia tunavyosafisha huku wakiendelea na shughuli zao, Angalia wale wavuvi kwenye mitumbwi yao wanaendelea na kazi zao na wao ndo wachafuzi wakubwa huko baharini na nchi kavu. “Alisema.

Mpina amemtaka mkuu wa wilaya hiyo kuwawajibisha viongozi walioko chini yake kwa kosa la uzembe wa ufuatiliaji wa sheria ya mazingira kabla hajawajibishwa yeye. “kiongozi mzembe afukuzwe kazi kabla haujafukuzwa wewe na kuingia kwenye matatizo.” Alisisitiza naibu waziri Mpina.
Hata hivyo Naibu Waziri Mpina alimpongeza mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Paul Makonda kwa kuanzisha kampeni ya upandaji miti maarufu kama ‘’MTI WANGU’’ na kuwashauri wakazi wa jiji kushiriki Katika siku ya uzinduzi na kuahidi kuwa pamoja nao siku hiyo.

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bw. Hashim Mgandilwa ameelezea jitihada za usafi wa mazingira katika mji wa kigamboni ikiwa ni pamoja na mashindano ya usafi wa mazingira na kuwataka wakazi wa kigamboni kuongeza jitihada za kutosha kuiweka kigamboni safi.
Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi ni siku maalum ya usafi ikiwa ni katika kutekeleza agizo la Rais la Usafi wa mazingira ambapo mwezi huu kitaifa imefanyika Kigamboni.
 Naibu waziri wa Nchi ofis ya makamu wa rais muungano na mazingira Mh.Luhaga Mpina akifanya usafi na wananchi wa wilaya ya kigamboni katika kutekeleza agizo la Mh. rais la kila mwisho wa mwezi kufanya usafi.      
Naibu Waziri wa Nchi ofis ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akiwa na wananchi wa kigamboni waliojitokeza kwaajiri ya kufanya usafi katika fukwe za kigamboni                      
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina akiongea na waandishi wa habari,hawapo pichani mara baada ya kumaliza kufanya usafi katika fukwe za wilaya ya kigamboni.