Na Dotto Mwaibale

KAMATI ya maandalizi ya shindano la Lete Raha Miss Kinondoni 2016 imemtangaza Diana Edward kuwa mlimbwende wa wilaya hiyo baada ya kuibuka mshindi katika shindano lililofanyika Hoteli ya Denfrances iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam jana.

Edward aliibuka mshindi baada ya kuwabwaga washiriki wenzake 20 waliokuwa wakiwania taji hilo ambapo nafasi ya pili ilichukuliwa na Regina Ndimbo huku ya tatu ikichukuliwa na Sia Pius ambapo Happyness Munisi akishinda nafasi ya utanashati.

Akizungumza wakati wa mchakato wa kutoa zawadi Mratibu wa shindano hilo, Rhamat George alisema asilimia 10 ya mapato yaliyopatikana katika shindano hilo yatakwenda Wilaya ya Kinondoni kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa ikiwa ni kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli ya kuhakikisha kila mwanafunzi anapata elimu bure katika mazingira bora.

Katika shindano hilo washindi waliofanikiwa kuingia tano bora wataingia moja kwa moja katika kinyang'anyiro cha kumsaka mlimbwende wa Tanzania.Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd kupitia bia ya Windhoek Lager na Draught pamoja na Gazeti la Lete Raha na wadhamini wengine.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift Msuya alisema Serikali itaendelea kuunga mkono mashindano hayo ambayo yamekuwa yakitoa ajira na kuibua vipaji vya watoto wa kike.

Shindano hilo lilipambwa na burudani kutoka kwa mwanamuziki wa muziki wa dansi Christian Bella na kundi la sanaa la Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd.
Malkia wa Kinondoni 2016 Diana Edward ndiye huyu hapa.
Lete Raha Miss Kinondoni 2016, Diana Edward (katikati), akipunga mkono baada ya kutangazwa kuwa mshindi Dar es Salaam jana. Kulia ni mshindi wa pili Regina Ndimbo na kushoto ni mshindi wa tatu, Sia Pius.
Mgeni rasmi wa shindano hilo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift Msuya (katikati), akikabidhi zawadi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...