*Na Anaclet Mkireti, _Economic Bureau_*

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe  (pichani) amedhihirisha kuwa  ameshikiwa akili na wafanyabiashara wenye agenda zao kwa kuuliza swali la kiuchumi bila utafiti. 
Akiuliza swali kwa Waziri Mkuu, Mbowe alidai eti uchumi wa Tanzania umedorora akitaja nyanja mbalimbali kushuka kama vile bandari, utalii  na mauzo ya nje.

Hata hivyo ukweli (facts) zinaonesha ama Mbowe anakabiliwa na athari za kutumia muda mwingi kujenga ukuta badala ya kusaka usahihi wa Takwimu au waliompa swali hawakufanya utafiti.
Nikiwa mchumi nafahamu kwamba uchumi haujengwi na sekta moja.Zipo sekta anuai na muhimu ambazo zikikua wachumi tunaamini uchumi uko imara.
Wakati Mbowe akitoa hoja hiyo bila takwimu bali porojo tu takwimu za wazi na ambazo hata sisi kama watafiti tunazo zinaonesha kama ifuatavyo;-



1.Mapato ya mwezi yameongezeka kutoka  wastani wa Sh. bilioni 900 mwaka jana hadi Trilioni 1.158 Sept., mwaka huu;



2.Pamoja na mizigo kupungua Bandarini kwa sababu zinazogusa dunia nzima bado mapato yamepanda kutoka wastani wa bilioni 300 kwa mwezi hadi Bandari kukusanya wastani wa Bilioni 500 ilipofika Mei 2016 kutokana na utawala wa Rais Magufuli kuzuia mianya ya ukwepaji kodi;



3. Uzalishaji wa umeme katika nusu ya kwanza ya 2016 umepanda kwa asilimia 14.5 na unatarajiwa kuongezeka zaid katika nusu ya pili ya 2016;



4.Idadi ya watalii, siku wanazokaa nchini na fedha zinazoingia Serikalini imeongezeka katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita licha ya kodi mpya zilizotangazwa;



5. Uzalishaji wa saruji umeongezeka kwa asilimia 7 baada ya Dangote kuanza kuzalisha Mtwara na kusababisha bei kushuka-jambo muhimu katika sekta ya ujenzi;



6. Uagizaji wa malighafi za viwanda kutoka nje umeongezeka kwa asilimia 19.4;
7. Mauzo ya bidhaa za viwanda nje yameongezeka kwa asilimia 15.6 tofauti na Mbowe anavyotaka tuamini ni kama vile uzalishaji nchini umekufa kabisa;
8.Pamoja na kuendelea kupotoshwa juu ya kukua deni la Taifa ukweli ni kwamba kiuchumi kwa Tanzania kuendelea kukopa maana yale ni kwamba nchi ina uchumi imara na unaokubalika kimataifa ndio maana taasisi za kimataifa na hata Benki ya dunia bado wanaridhia ikope.Tanzania inakopesheka.Marekani pia inakopa.

9. Kampuni za simu zimelipa kodi kubwa zaidi Serikalini katika robo ya kwanza ya mwaka huu wa Bajeti baada ya kuwa wanalipa kiduchu huko nyuma;

10.Miradi ya uwekezaji au wawekezaji kwa ujumla imeongezeka zaidi Tanzania katika miezi 8 iliyopita kuliko wakati wowote nchini tofauti na Mbowe anavyodai eti wawekezaji wanakimbia.
Siku nyingine Mbowe aombe msaada wa watafiti hasa anapotaka kuhoji mambo ya kitaalam kwa sababu uchumi ni sayansi na sio siasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mh! kazi kweli kweli !

    ReplyDelete
  2. sijui huyu anayejiita mchumi ana elimu na uzoefu kiasi gani. ngoja niendelee kufanya mahojiani wa wabobezi wakiwa kwenye comfort zone maana siku hizi kila mtu mwoga wa kusema ukweli mbele za watu which is a very un tanzanian.

    ReplyDelete
  3. Mikausho MikaliSeptember 09, 2016

    Mtoa ameongea kitaalamu sana na yuko sahihi kwa asilimia mia moja.Ila kwa mapato yanayopatikana Bandarini kwa sasa kwa wastani wa makontena yanayoingizwa 2000 ukilinganisha na idadi inayosemwa kuwa ilikuwa inaletwa zamani 40000 basi bandari ni eneo muhimu litakaloweza kututoa sana kama tukiwekeza vizuri pale.Kuna nchi ambayo zimepiga hatua na zinategemea sio sekta nyingi na mfano mzuri ni Mauritius au Ethiopia

    ReplyDelete
  4. The mdudu, Du asante sana mdau wa uchumi hata sisi walala hoi tunayaona hayo kwa macho mfano mzuri na wawazi kabisa ni ule ujenzi wa kijiji cha wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar ambao unajengwa usiku na mchana huyo ndio JPM bwana go go JPM go go Tanzania

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...