Upo mjadala unaoendelea na kufukuta kuhusu uamuzi wa Serikali kupeleka Muswada wa Sheria Bungeni kufanya marekebisho katika Sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Muswada huo sijauona na haujawekwa hadharani. Hata hivyo, lililopenyezeka katika vyombo vya habari ni taarifa ya azma hiyo ya Serikali iliyotamkwa katika kikao cha Serikali na wadau kuwa Muswada huo utafuta FAO LA KUJITOA.

Nimefuatilia mjadala huo na kuisoma barua ya wazi ya vyama vya wafanyakazi kwa umma ikilaani vikali nia hiyo ya Serikali na muswada. Nikasikia na kusoma tena kauli mbalimbali za Serikali na Mamlaka ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kuhusu azma hiyo na mambo mengine mengi yanayoambatana na muswada unaondaliwa. Kwa maelezo hayo, muswada huo una mambo mengi zaidi ya kinachoitwa fao la kujitoa. Aidha, maelezo yao ni kuwa muswada wenyewe haujakamilika isipokuwa ni hatua ya maoni tu.
 Ninachokiona kwa haraka haraka ni kuwepo kwa ombwe la taarifa katika suala hili jambo linalofanya mjadala wenyewe kwenda harijojo. Ombwe hili litafanya hata muswada wenyewe ukitolewa tushindwe kuujadili vizuri  na kwa nafasi. Kwa sababu hiyo, nimejitolea kuchokoza mjadala kwa kuyaweka bayana mambo 10 ya msingi ya kuyaelewa kuhusu hifadhi ya jamii kama ninavyoyainisha hapa chini...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...