THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

HOSPITALI YA KISASA YA MUHIMBILI-MLOGANZILA KUANZA KUTOA HUDUMA JANUARI 2017.

 Mwonekano wa Jengo la Hospitali ya Kisasa ya kufundishia wataalamu wa afya na kutoa huduma za afya.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili, Profesa Ephata Kaaya akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea katika Hospitali ya Kisasa ya kufundishia wataalamu wa afya na kutoa huduma za afya jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili, Dkt. Said Aboud.

 Baadhi ya Madaktari na wakuu wa vitengo wa Hospitali ya Kisasa ya kufundishia wataalamu wa afya na kutoa huduma za afya wakiwa katika mkutano jijini Dar es Salaam leo.
Mtaalamu wa Tehama, Andrew Fundamali akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari walipotembelea katika mitambo ya tehama katika hospitali hiyo.
  Wandishi wakipewa maelekezo walipotembelea katika chumba chenye mashine za MRI na CT scan.
 Daktali wa kitengo cha Koo, pua na masikio akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

UJENZI wa Hospitali ya kisasa ya kufundishia wataalamu wa afya na kutoa huduma -shirikishi ya Muhimbili iliyopo Mbezi eneo la Mloganzila jijini Dar es Salaam yakaribia kumalizika kufunga vifaa tiba na kuanza kufanya kazi ifikapo Januari 2017 itaanza kutoa huduma mbalimbali  kwaajili ya kufundishia fani za afya na kutoa huduma ya matibabu yapasayo kwa wagojwa.

Hayo yamesemwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili, Profesa Ephata Kaaya wakati waandishi wa habari  walipotembelea katika hospitali hiyo ya kisasa ya kufundishia wataalamu wa  afya na kutolea huduma mbalimbali za afya hapa nchini.

Amesema kuwa eneo la hospitali hiyo linaukubwa wa ekari 3800 na inauwezo wa kuchukua vitanda 571 na ipo umbali wa Kilomita 25 kutoka jijini Dar es Salaam pia inauwezo wa kuchukua wanafunzi 4000 ikitofautishwa na waliopo sasa ni 1500 tuu.

 Profesa Kaaya amesema kuwa upungufu wa wataalamu wa afya katika mikoa na wilaya hapa nchini ndiko kulikosababisha  Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi ya Muhimbili kuanza kutafuta maeneo yakupanua na kujenga hospitali ya Kisasa ya kufundishia wataalamu wa afya na kutoa huduma za afya.

Profesa Kaaya amesema kuwa wagojwa watakaopelekwa katika hospitali hiyo ni wale watakaokuwa wamepewa rufaa kutoka hospitali za mikoa mbalimbali ya hapa nchini.

Amesema kuwa jengo hilo lina sehemu mbili na linaghorofa tisa za juu na ghorofa moja chini ya ardhi linaeneo la Mapokezi, Idara ya Utawala, Idara ya Mahesabu, Phamasia, Idara ya Mionzi, Idara ya wagonjwa wa dharula pamoja na upasuaji wa Dharala, Idara ya afya ya kinywa na meno,chumba cha wagojwa  mahututi, chumba cha kusafisha figo na wadi ya kujifungulia.


Eneo jingine ni vyumba vya kufundishia wanafunzi maktaba ya hospitali, ofisi ya mkuu wa hospitali, ofisi za madaktari na waalimu, ofisi ya Muuguzi Mkuu na kituo cha kopyuta.