Na Kamati ya Hijja ya Tanzania.
Ibada ya hijja imemalizika rasmi katika mji wa Makkah na Madina na mahujaji wa dini ya kiislamu zaidi ya milioni 2 kutoka nchi zipatazo 164 wameanza kurejea makwao walikotoka.
Ibada ya mwaka huu imekuwa ya mafanikio kwa kumalizika salama. Hii ni kutokana na Serikali ya Saudi Arabia kuwa na mipango madhubuti kwa kuimarisha miundombinu, usafiri, ulinzi na usalama na kurekebisha dosari zilizojitokeza mwaka jana.
Maeneo ya misikiti yote miwili ya Makkah na Madina yaliimarishwa na yanaendelea kujengwa ikiwa ni pamoja na kupanuliwa ili kuongeza nafasi za kutosha kufanyia ibada.
Mahujaji kutoka Tanzania wapatao 2,000 wako salama na wao ni miongoni mwa walioshiriki katika ibada na sasa wako njiani kurejea Tanzania. Hatua zilizochukuliwa na mamlaka za ulinzi za Saudi Arabia ni pamoja na kuhakikisha kuwa makundi ya misafara ya mahujaji hayagongani kati ya wanaokwenda na wanaorudi, njia mbalimbali zilikuwa zikifungwa na kufunguliwa ili kuruhusu misafara kwenda uelekeo mmoja bila kukutana. Hatua hii ilisaidia kuepusha ajali kama iliyotokea wakati wa ibada ya hijja ya mwaka 2015.
Mahujaji wa Tanzania walipokuwa katika misafara ya majaribio (rehearsal) ya kujua njia kuelekea Jamarat eneo la Mina.      

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...