THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

INTRODUCING "SALOME" BY Diamond Platnumz ft Rayvanny


Sallam kutoka WCB ameonyesha baadhi ya nyaraka ambazo zimewapitia kibali cha kutumia sehumu za wimbo ‘Maria Salome’ wa Saida Karoli katika wimbo mpya wa Diamond, ‘Salome’.
saida-karoli

Wimbo ‘Maria Salole’ wa Saidi Karoli ni miongoni mwa nyimbo za asili zilizofanya vizuri miaka ya 2000.Hali hiyo iliufanya uongozi wa Diamond kuzungumza na uongozi wa Saida Karoli ili upate kibali cha kutumia sehemu za nyimbo hiyo.
“Tunakushukuru sana uongozi wa Saida Karoli na mzee Felician Mutakyawa kutupa haki na baraka zote kutumia wimbo wa Maria Salome,” aliandika Sallam instagram. “Tunatambua kwamba nyimbo hii itaendelea kuwa moja ya nyimbo bora kuwahi kutoka katika nchi ya Tanzania,”
Diamond kupitia wimbo huu amerudi tena katika nyimbo za asili baada ya kufanya vizuri na wimbo ‘Mdogo Mdogo’ miaka miwili iliyopita.
Pichani juu anaonekana Diamond na Rayvanny wakiwa na Mzee Felician Mutakyawa wakati wa kusaini makubaliano ya kutumia sehemu ya wimbo huo wa 'SALOME' ambao umebamba kila kona.
CHANZO: BONGO FIVEKuna Maoni 6 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Hakuna mwengine zaidi ya Diamond.

 2. Anonymous Anasema:

  Aisee Naseeb, hapa ndipo anapowaacha mbali artists wengine wa Bongo kwa ubunifu wake.... Diamond hakika yupo juu, wengine watafuata nyuma tuu, watake wasitake.
  Endelea na uzi huo huo!

 3. Anonymous Anasema:

  jamaa anajua sana

 4. HK Anasema:

  Masha Allah! Kwa kweli hii 'version' ya 'Maria Salome' iliyoimbwa na Diamond Platnumz ft Rayvanny, ipo very 'classic'. Hakika mnastahili pongezi za pekee kwa kazi nzuri, kuanzia midundo (muziki) , uchezaji na hata ujumbe 'makhsusi' uliyomo katika wimbo huo, kwa kweli wenye wivu wajinyonge tu. Hakika mnastahili sifa na pongezi za pekee 'crew' nzima ya WCB kwa ushirikiano wenu.

 5. sharifu masoud Anasema:

  Safi sana,, ila kama haujasoma magazeti ya leo basi SOMA HAPA

 6. kadala Anasema:

  Sanaa ni ubunifu, mmeutendea haki huu wimbo, mmewaacha 'kodo', hongereni sana Diamond na team nzima ya WCB