THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Jamii yatakiwa kuwa mstari wa mbele kupiga vita ndoa katika umri mdogoMwashungi Tahir Na Khadija Khamis Maelezo Zanzibar 8-9-2016

Jamii inatakiwa kuwa mstari wa mbele kupiga vita ndoa katika umri mdogo kutokana na athari ambazo zinazoweza kujitokeza na kuhatarisha maisha ya mama na mtoto.

Hayo yameelezwa na Mwanasheria wa Zafela Salma Suleiman huko katika jengo la malaria Mwanakwerekwe kwenye semina ya kupinga ndoa za utotoni na udhalilishaji wa wanawake na watoto iliyowashirikisha wazazi, walimu wa vya madrasa pamoja na masheha.

Amesema jamii ipewe elimu zaidi ili ndoa hizo zisiweze kuendelea ambazo zinaweza kuhatarisha maisha ya watoto pamoja na kuzidisha umaskini katika jamii.

Aidha watoto chini ya umri wa miaka 18 viungo vyao vinakuwa bado havijakomaa kwa kuweza kujifungua kwa njia salama hivyo kunauwezekano mkubwa wa kupata matatizo wakati wa kujifungua .

Alieleza jamii ielewe faida na hasara za ndoa hizo kwani kupelekea ongezeko la watoto wa mitaani , pamoja na maradhi ya zinaa ambayo hupelekea kupata maradhi ya maambukizi .

Pia alielezea kuwa serikali imetunga sheria ya elimu, na sheria za makosa ya jinai ya mwaka 1984 ambayo imetoa adhabu kwa mtu yeyote ambae atamfanyia mtoto suala la udhalilishaji chini ya umri huo.

“Sheria ya elimu inamfanya mtoto atakapo pata uja uzito baada ya kujifungua ndani ya miaka miwili kwa wakati wowote anaruhusika kurudi kuendelea na masomo yake , “Alisema Salma .

Vile vile kwa mzazi au mlezi ambae atachukua hatua ya kumuozesha mtoto mwenye umri mdogo ataingia hatiani kwa mujibu wa sheria ya kosa la jinai na kutozwa faini kwa mujibu wa makosa ,kisheria.

Sambamba na hayo mwanasheria huyo alisema kesi za udhalilishaji zinaongezeka siku hadi siku kutokana na uzorotaji wa kutolewa hukumu kwa kesi hizo na kuongezeka kwa malimbikizo ya kesi hizo.

Akitoa msisitizo kwa wazazi na walezi kuepuka adhabu za kuwanyima vyakula , kumpiga kupita kiasi kunaweza kukampelekea uzururaji wa mitaani na kupata udhalilishaji wa kubakwa

Nae sheha wa shehia ya Mpendae Haji Seti ameitaka jamii isivunjike moyo wakati inapotokea kesi ya ushalilishaji kwenda mahakamani kwa kila siku hadi itapotolewa hukumu ya kesi hiyo

“Wazazi pamoja na mashahidi huvunjika moyo kwa muda mwingi unaotumika kwa kutolewa hukumu kwani daktari tayari amekwisha thibitisha ushahidi wake lakini tatizo ni kwa waendeshaji mashtaka wanataka ushahidi usio na shaka jambo ambalo halitowezekana.”walisema baadhi ya wazee hao .

Amewataka wazazi wawe mstari wa mbele kwa kufatilia kesi hizo pindipo zinapotokea hadi pale mahakama inapofikia hatua ya kutoa maamuzi yaliyo sahihi.