Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maofisa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) inamshikilia Dereva Bw. Emanuel Bisama (37) ambaye ni mkazi wa Kimara Suka Dar es Salaam,kwa kosa la kusafirisha magunia mawili ya mkaa ambayo baada ya kupekuliwa ndani yake kulikutwa na viroba viwili vyenye uzito kilo 50 kila kimoja vikiwa vimejaa bangi.

Akizungumza jana na Waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Pwani , ACP. Bonaventura Mushongi alisema Mtuhumiwa ambaye ni dereva wa gari lenye namba za usajili T876 DDL aina ya DAF Leyland Bw. Emanuel Bisama (37) alikamatwa Septemba 21 saa 4.00 asubuhi katika kata ya Vigwaza tarafa ya Chalinze mkoa wa Pwani katika Bara bara kuu ya Morogoro akitokea Tunduma na kwa sasa yupo mbaroni kwa mahojiano licha ya kukana kuwa hakujua kilichomo ndani ya magunia hayo.

Kamanda Mushongi alisema walifanikiwa kumkamata wakiwa katika Operesheni ya Ukaguzi wa mazao ya Misitu katika Barabara kuu ya Morogoro hadi Dare Salaam, aliongeza kuwa Dereva huyo wa gari amefunguliwa kesi CHA/RB/3039/2016 kwa kosa la kupatikana na bangi

Kwa upande Wakala wa Hudumza Misitu Tanzania (TFS) Kaimu wa Kanda ya Pwani Bw. Jonathan Mpangala alisema kuwa Mtuhumiwa huyo amefunguliwa kesi ya pili yenye CHA/RB/5113/2016 kwa kosa la kumiliki na kusafirisha mazao ya misitu bila kibali kwa sheria ya misitu namba 14 ya 2012 kifungu 88 na 89.

Alisisitiza kuwa Operesheni ya kukamata usafirishaji wa mazao ya misitu bila vibali itakuwa ya kudumu baada ya kuona magari mengi hasa makubwa yakiwa yamepakiwa magunia ya mkaa kuanzia mawili hadi matano ambayo yamekuwa yakioneka waziwazi hata ukiwa barabarani namengi yakiwa hayalipiwa ushuru wa Serikali kuu na hata magari mengine yakiwa hayajalipiwa ushuru wa Halmashauri

Askari polisi wa kituo cha polisi cha Chalinze akionesha viroba viwili vya bangi vyenye uzito wa kilo 50 kila kimoja vilivyokamatwa jana katika Operesheni ya kuthibiti utoroshaji wa mazao ya Misitu yasiyo na kibali katika kata ya Vigwaza tarafa ya Chalinze mkoani Pwani katika Bara bara kuu ya Morogoro wakitokea Tunduma wakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T876 DDL aina ya DAF Leyland ( Picha na Lusungu Helela- Afisa Habari Maliasili na Utalii) 
Viroba viwili vya bangi vyenye uzito wa kilo 50 kila kimoja vilivyokamatwa jana katika Operesheni ya kuthibiti utoroshaji wa mazao ya Misitu yasiyo na kibali katika kata ya Vigwaza tarafa ya Chalinze mkoani Pwani katika Bara bara kuu ya Morogoro vikitokea Tunduma vikiwa kwenye gari lenye namba za usajili T876 DDL aina ya DAF Leyland ( Picha na Lusungu Helela- Afisa Habari Maliasili na Utalii)

Kaimu mkuu wa Kanda ya Pwani wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Bw. Jonathan Mpangala akiwaonesha waandishi wa habari gari lililokuwa limebeba magunia mawili ya mkaa ambayo ndani yake kulikuwa na viroba viwili vilivyojaa bangi vyenye uzito wa kilo 50 kila kimoja ( Picha na Lusungu Helela- Afisa Habari Maliasili na Utalii) 
Moja ya Kiroba kilichojaa bangi chenye uzito wa kilo 50 kilichokamatwa jana katika Operesheni ya kuthibiti utoroshaji wa mazao ya Misitu yasiyo na kibali katika kata ya Vigwaza tarafa ya Chalinze mkoani Pwani katika Bara bara kuu ya Morogoro kikitokea Tunduma kikiwa kwenye gari lenye namba za usajili T876 DDL aina ya DAF Leyland (Picha na Lusungu Helela- Afisa Habari Maliasili na Utalii) 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...