Viongozi wapya wa KIDIFA wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Hassan Ngubege
 Mwenyekiti wa KIFIDA aliyemaliza muda wake, Hassan Ngubege akimkabidhi Mwenyekiti mpya wa chama hicho Jesse John katiba ya chama hicho.
 
 
Na Mwandishi Wetu,Kisarawe
MTANGAZAJI nguli wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jesse John amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kisarawe (KIDIFA) katika uchaguzi uliofanyika jana.
Jesse ambaye aliupata uongozi huo katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa aliibuka kidedea baada ya kupata kura 32 na kumshinda mpinzani wake Karim Wenge aliyepata kura 21.
Katika uchaguzi huo Mohamed Lubondo alichaguliwa kuwa Katibu baada ya kupata kura 30 na kumshinda Francis Mkamba aliyepata kura 27.Katibu Msaidizi alichaguliwa kuwa Amosi Kisebengo, Makamu Mwenyekiti alichaguliwa kuwa Abdul Mogella.
Wasimamizi wa uchaguzi huo kutoka Chama Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA), Mweka Hazina wa KIDIFA alichaguliwa Iddo Mtangaze na Mweka Hazina Msaidizi alichaguliwa kuwa Sadiki Nasoro.
Mwakilishi wa klabu kutoka Tarafa ya Mzenga alichaguliwa kuwa Suleiman Mahenge, kutoka Tarafa ya Sungwi alichaguliwa Abdallah Kuga na Mwakilishi wa klabu alichaguliwa kuwa Ally Madega na Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa mkoa alichaguliwa kuwa Mohamed Masenga.
Mwenyekiti wa KIDIFA aliyemaliza muda wake Hassan Ngubege akimkarisha Jesse kushukuru wajumbe aliwataka viongozi wapya kufufua matumaini ya vipaji vya vijana katika soka wilaya ya Kisarawe kwa kuanzisha mashindano mbalimbali yenye lengo la kutafuta vipaji.
Jesse akiwashukuru wajumbe hao aliahidi kushirikiana na wadau wa soka ndani na nje ya wilaya hiyo kupata timu ya wilaya itakayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom kama timu nyingine zinashiriki mashindano hayo.
Mwenyekiti Jesse alisema wilaya ya Kisarawe ambako yeye ni mzaliwa wa asili alisema anaamini vijana wengi hawajapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao hivyo atatumia miaka minne ya uongozi kuzalisha vijana wazuri katika soka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nakupongeza 'mate' wangu kwa jitihada zako katika masuala mazima ya michezo na utangazaji kwa jumla. Pia hongera sana kwa kuchaguliwa kushika wadhifa huo. Kwa kweli umejaaliwa kipaji cha pekee khususan katika suala zima la utangazaj, nakumbuka tangu ukiwa Chuoni miaka ile ya 1990's uliweza kukidhihirisha kipaji chako hicho na hata katika masuala mazima ya 'kispoti' kwa kweli abadan hukubakia nyuma kwa jumla, Am so proud of you and keep it up!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...