THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

JIFUNZE MCHEZO WA KARATE: Zijue tofauti za mitindo ya karate na sanaa nyingine kuu za mapambano 7 toka Japan

Sensei Rumadha Fundi akifanya "Suparinpei Kata"
Hapana  budi , bali ni furaha kuielimisha jamii ya wapenda karate na sanaa mbali mbali za mapambano na kujilinda zenye asili ya Japan. Ingawa ni vigumu kuchambua historia zake zote kiundani, bali muktasari wake unawezekana na kuipa jamii ya mapenzi ya hizi sanaa mpambazuko wa ufahamu kuhusu sanaa hizi za Kijapan. Katika muktasari huu, itaongelewa zile sanaa halisi ( original) au shina lake na siyo matawi ya baadhi ya sanaa hizi yaliyojitokeza baada ya waanzilishi kufa na wanafunzi kuanzaisha mitindo yao.

1. JUDO 2. KENDO 3. AIKIDO 4.JUJUTSU 5. KEMPO  6. KOBUDO 7. KARATE.

1. Judo: Yenye maana “ Mwenendo wa sanaa ya upole”Mieleka  ilianzishwa mwaka 1882, kama mazoezi ya mwili na fikra kuimarisha mwili kuwa madhubuti au imara. Mwanzilishi wa sanaa hii ya Judo ni mkufunzi wa Buddha “Buddhist” Jiogoro Kano, kwenye hekalu la “Eisho-ji”Buddha kama dojo yay a Judo mjini Tokyo. Papo hapo ndipo na miaka miwili baadae kuanzisha chama cha Judo kiitwacho “Kodokan”kikimaanishe au tafsiri, “Sehemu ya kuonyesha njia”. Kipindi hicho, Sensei Kano alikuwa bado hajapewa “ Menkyo” au kumuenzi na cheo cha master. 

2. Kendo: Yenye maana “ Njia ya upanga” ni sanaa nyingine pia ya Japan yenye kutumia mapanga kwa kujilinda na kushambulia pia.

3. Aikido: Ni saa ya kisasa pia ilianzishwa na  Morihei Ueshiba, ikiwa na maana, “ Njia ya kuunganishanisha nafsi na roho”, ama pia “ Njia ya kuunganisha nguvu za maisha”. Master Ueshiba , alibuni mbinu hizi za kujilinda kutumia nguvu za  kumrusha  mpinzani wako wakati akigoma na kuigeuza nguvu yake mwenyewe kumzatiti na kupinda viungo kummiliki mpizani. Aikido, ilianzishwa mnamo miaka ya 1920 ikiwa nimoja ya ndoto zake toka katika dini yake ya  kidini ya “Omoto - Kyo”. Leo Aikido, anafundishwa duniani kote na ina matawi tofauti ya mfumo wakufundisha.
Sensei Rumadha Fundi akifanya "Sai Kata"

4. Jujutsu: Jina Jujutsu, halikutolewa hadi hapo mnamo mwanzoni mwa karne ya 17, ikiwa mbinu zake zime sambaa kiujumla kama miekeka, na hali kadhalika kunyongana na kikiri kiri na kiujumla ni mzunguuko kamili wa kujilina kwa karibu na mpinzani kimwili kuwa pamoja au mapambano ya karibu ya kugusana. Kiujulma ni kwamba, Jujutstu ina husisha mbinu nyingi tofauti zikiwemo kushambulia, ngumi, kumrusha adui, kumbana adui, kunyonga adui, na hata mieleka pia.

Sanaa hii inachimbuko lake Japan na baadae kutambulishwa Brazil mwaka 1914 na sensei Mitsuyo Maeda, ambae moja ya wanafunzi wake toka Brazil ni Sensei Carlos Gracie na familia yake walikuja endeleza sanaa hii kupitia michezo na kujulikana kama “Gracie Jui Jutsu” au pia maarufu kama “Mixed Martial Arts”. Upo ushawishi mwingi sana toka katika mfumo wa Jigoro Kano Judo, ambaye ndiyo “Baba wa Judo” Maste Kano ndio aliyekuwa mwalimu wa Sensei Mitsuyo Maeda na kusambaza Ju Jutsu hadi Brazil.

5. Kempo: Kutokana na historia yake, Kempo ililetwa china na mwanzilishi wa Zen, Boddhidarma mnamo karne ya 1500. Baada ya kuondoka India kufundisha “Buddhism” China. Safari ya Buddha, iliishia katika hekalu la Songshan, kwenye Hekalu maarufu la “Shaolin”, ambapo leo kunajulikana kama jimbo la “Henan”, na baadae mbinu hizo kuenea nchi yote ya China.

Hii sanaa ya Kempo, yenye maana ya “Boxing”, imejigawa katika makundi matatu tofauti na miaka iliyopisha  kwa wakati wake. Sanaa hii ili pelekwa katika visiwa wa Okinawa na inauhusiano mkubwa sana na mtido wa “Shuri Te, Shorinji Ryu  na Shorin Ryu, Shito Ryu, Motobu Ryu” pia. Sababu ndio mtindo aliotoka nao Master Gichin Funakoshi (Shuri Te) toka Okinawa kwenda Japan ya bara 1922, na baadae kuitwa Shotokan Karate.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI