Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akizungumza na Wananchi walio fika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kupata vipimo na kupatiwa ushauri na Madaktari kutoka Hospitali Mbalimbali Jijini Dar es Salaam,hapo jana,ambapo leo RC Makonda ameongeza Siku Mbili (2), zoezi la Upimaji Afya bure

"Awali ya yote niwapongeze wananchi wangu wa mkoa wa Dar es Salaam walioonyesha mfano mzuri wa kujali afya zao na jamaa zao kwa kuitikia fursa ya wito wangu wa kupima afya bure, lengo likiwa ni kuhakikisha tunazijua vyema na mapema hali za afya zetu ili tuwe na nafasi nzuri zaidi ya kushughulikia changamoto zozote zinazobainika ama zinazoweza kujitokeza kwa mujibu wa maelezo ya watalaamu.
"Kitakwimu, wataalamu wetu kutoka taasisi na hospitali mbalimbali ambazo ninashirikiana nazo walipokea zaidi ya wagonjwa 14,000, idadi ambayo ilitupa moyo na faraja sambamba na changamoto ndogondogo za hapa na pale kutokana na ukweli kuwa hatukuwa na matarajio ya idadi kubwa kiasi hiki, jambo ambalo kimsingi lilipelekea zoezi kushindwa kukamilika Kwa muda uliokuwa umepangwa hapo awali.
"Kwa msingi na nia yangu ile ile ya kuhakikisha kila mwananchi aliyefika viwanja vya mnazi mmoja anapatiwa huduma, nimeona ni vyema niongeze siku mbili (2) za muendelezo wa upimaji wa afya ili kumpa nafasi kila mwananchi aliyefika ktk viwanja vya mnazi mmoja kupata huduma. Pili, imenibidi niongeze nguvu kwa kumuomba waziri wetu wa ulinzi Dr. Hussein Mwinyi kutupatia madaktari na wauguzi kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ambaye amelipitisha ombi hilo na hivyo kutuongezea madaktari wengine pamoja na wauguzi wasiopungua 90 ambao wataungana nasi kesho, hivyo kukamilisha jumla ya madaktari na wauguzi 240, idadi ambayo nina uhakika itatuwezesha kumuhudumia kila mtu na kwa wakati.

"Mwisho ningependa kuwaomba wananchi wote hasa waliofika Mnazi mmoja kuendelea kuwa wavumilivu ili kuwapa moyo Madaktari wetu kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya. Mimi RC wenu naendelea kushirikiana nanyi bega kwa bega na sitawaacha" amsema RC Makonda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...