Na MatukiodaimaBlog.
SERIKALI  ya  mkoa  wa  Iringa   imepongeza  msaada mkubwa uliotolewa na kampuni ya  Asas  ya  mkoa hapa wa ujenzi wa jengo la  kituo  cha  damu  salama  cha  kisasa na ujenzi wa  jengo la  watoto  wanaozaliwa  njiti katika  Hospitali  teule ya  mkoa  wa  Iringa pamoja miradi  itakayogharimu zaidi ya  Tsh  milioni 400

Katika  taarifa   iliyosomwa na mganga  mkuu  wa  Hospitali ya rufaa ya  mkoa wa Iringa Dr Robert salim wakati wa  hafla ya  uwekaji wa jiwe la msingi   katika miradi hiyo leo  mbele ya mgeni rasmi   mkuu wa  mkoa wa Iringa  Amina Masenza  alisema  kuwa awali  uongozi wa hospitali  hiyo  ulimwandikia  barua  mfanyabiashara    huyo  ili  kusaidia  msaada wa kontena ambalo  lingetumika katika  kituo cha benki ya  damu salama ila mfanyabiashara   huyo alijitolea  kujenga jengo  hilo la  kisasa na kuongeza msaada wa jengo la watoto  wanaozaliwa  njiti .

“Kutokana na agizo la Serikali la kuanzisha Benki za damu salama katika Mikoa..... Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na Mfadhili  Salim F. Abri Mkurugenzi wa Kampuni ya ASAS iliona ni vyema kujenga jengo la Kituo Kidogo cha damu salama katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ili kufikia azma hiyo. ...Hospitali ilimuomba Mfadhili huyo atoe msaada wa “Container” kwa ajili ya shughuli hiyo, lakini Mfadhili kwa kuona umuhimu wa huduma ya damu salama katika Mkoa aliomba apewe ramani ili ajenge kituo hicho badala ya kutumia“Container”.”alisema

Dr Salim alisema  kuwa Hospitali   hiyo kabla ya  mfanyabiashara   huyo  kujitolea  ujenzi wa  jengo  hilo  kituo cha  kidogo  cha damu  salama  ulikuwa  ukitegemea  damu  kutoka  kituo  cha kanda  kilichopo  mkoani  Mbeya  ila  sasa  wataweza  kukusanya  damu  kupitia  kituo  hicho.

Alisema  kuwa lengo la mradi huu ni Kuboresha upatikanaji wa huduma za damu salama katika Mkoa wa Iringa kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya damu salama katika Vituo vya kutolea huduma za afya na kupunguza vifo vya Uzazi, Watoto wachanga, Watoto na Wahanga wa ajali za barabarani na kuwa lengo la Mkoa kwa mwezi ni kukusanya chupa 784 na kwa mwaka ni chupa 9,413 (units).

Hata  hivyo  alisema mahitaji ya damu kwa mwezi katika Mkoa ni chupa 700 (unit) na katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ni chupa 160-200 Units kwa mwezi kuwa tangu kituo kianze kutumika mwezi Februari,2016 Mkoa umekusanya chupa 2,065 (22%) hadi sasa.

“Tunakushukuru mkuu wa mkoa  kwa kukubali mwaliko wetu wa kuwa Mgeni Rasmi katika hafla hii ya kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Mfadhili wetu Salim F. Abri Mkurugenzi wa Kampuni ya ASAS ya Iringa. Katika hafla hii fupi tutakuomba uweke jiwe la Msingi katika Mradi wa jengo la Kituo Kidogo cha Damu Salama na Jengo la Wodi ya Watoto wachanga vyote  vikiwa ni  hisani  kutoka kwa mfadhili wetu  Salim F Abri “

Alisema kuwa ujenzi huo  unafanywa namkandarasi anayenga mradi huu ni Buyungu General Enterprise wa Iringa chini ya usimamizi wa  Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambaye amechangia kuchora ramani za jengo hili na kusimamia mradi mpaka ulipokamilika, mchango wake kama angelipwa ni Tshs.13,939,200.00.

Na kuwa  utekelezaji wa mradi ulianza kutekelezwa mwezi Novemba, 2014 na umekamilika mwezi Agosti, 2015. Jengo limeanza kutumika mwezi Februari, 2016. Pamoja na kujenga jengo hili Mfadhili pia ametoa msaada wa samani, mafriji makubwa 4 ya kutunzia damu na Computer 1 wenye thamani ya Tshs.30,000,000.00.
 
Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Amina Masenza (kushoto)  akimpongeza Salim Asas   (kulia) mara  baada ya  kuweka  jiwe la msingi katika miradi  mikubwa  miwili iliyofadhili   kampuni ya Asas ukiwemo  mradi wa jengo la  kituo cha  damu  salama Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa na jengo la  watoto  wanaozaliwa njiti yote yaliyofadhiliwa kwa zaidi ya Tsh milioni 400  na  kampuni hiyo ya  Asas ya  mkoa wa Iringa(picha na matukiodaimaBlog )
Damu  iliyochangiwa

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...