MENEJA Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti amesema  wanalo jukumu la kuhakikisha huduma wanazazotoa kwa ajili ya  Watanzania zinakuwa salama wakati wote ikiwa ni sehemu ya kuunga  mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kuhamasisha kutumia  njia za kieletroniki kwenye malipo ya fedha.
 
Corsaletti alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa  huduma mpya inayojulikana kwa jina la Airtel Money Tap Tap ambayo  inamuwezesha mteja wao anapotaka kununua mafuta kwa kutumia  kadi ya Airtel badala ya kutoa fedha taslimu akiwa kituo cha mafuta. 
 
Alisema wanahisi kwamba wanawajibu wa kufanya huduma zao kwa  usalama, senye ufanisi na rahisi zaidi kwa wateja wao na kufafanua ni  hatari kubeba fedha wakati wote maana ni rahisi kuhatarisha maisha.
 
Aliongeza kuwa ili kufanya jamii ya Watanzania inakuwa salama wakati  wote imeona kuna haja ya kuwa na huduma hiyo ambayo  itamuwezesha anayehitaji kununua mafuta kwenye vituo vya Puma  vilivyopo maeneo mbalimbali ya Dar es salaam wanatumia kadi za Airtel  kununua mafuta.
 
“Milango yetu iko wazi kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma zetu  na kuna jambo lolote ambalo tunaweza kulifanya ili jamii yetu  kuwa  salama wakati wote.Hivyo kuna umuhimu wa kuwa na matumizi ya  kadi ya Airtel katika kununua mafuta kwenye vituo vyetu vya  Puma,”alisema.
 
Akifafanua zaidi kuhusu huduma ya Airtel Money Tap Tap, Corsaletti  alisema chini ya utaratibu huo mtu yeyote aliyejisajili na huduma ya  Airtel Money atakuwa na uwezo wa kulipia bidhaa za Puma katika vituo  vyake vyote nchini kwa kutumia kadi  ya huduma ya Airtel Tap Tap   badala ya kutumia fedha kwa ajili ya huduma kama hizo.
 
“Kadi hii imeundwa kwa namna ambayo wakati wa kutumika kufanya  malipo , hupunguza fedha kwa kiasi cha malipo kutoka katika akaunti  ya Airtel Money ya mnunuzi kwenda kwenye akaunti  ya muuzaji. “Kadi hii itakuwa inauzwa kwa bei ya Sh 2, 000 kwenye vituo vyote vya  Puma Dar es Salaam na maduka yote ya Airtel Tanzania .Kuanzia mwakani kadi hii itakuwa pia inapatikana katika vituo vyote vya mikoani  ambavyo vipo chini ya Puma,”alisema.
 
Alitumia nafasi hiyo kueleza kuwa Puma Tanzania ina jumla ya vituo 46  nchini kote na kwa kuanza, vituo vyote vya Dar es Salaam vitakua  vinatoa huduma hiyo, hali vituo vingine vilivyosalia vitaunganishwa hivi  kuanzia mapema mwakani.“Lengo letu ni kuhakikisha kwamba aina yoyote ya biashara  tunayofanya, inafanyika kwa namna ambayo mtumiaji wa mwisho  anaridhika, na kubaki salama. 
 
“Tunaamini  hili kuwa jukumu letu kwa jamii popote wanapotumia  huduma zetu. Kwa kutumia kadi hii ya Airtel Money Tap Tap, mtu  hatahitaji kubeba tena hela tasilimu ili kupata huduma katika kituo cha  Puma,”alisisitiza.
  Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti kushoto na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso wakionesha mikataba yao pamoja na kadi ya Airtel Money Tap Tap mara baada ya hafla hiyo fupi ya kutiliana saini ya makubaliano hayo,hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Mafuta cha Puma Oysterbay,jijini Dar.
 MENEJA Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti kushoto na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso  wakiasini  mkataba wa makubaliano ya uuzaji wa mafuta kwa kutumia kadi ya Aiter Money Tap Tap , Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Mafuta cha Puma Oysterbay jijini  Dar es salaam.
 Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti kushoto na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso  wakibadilishana mikataba mara baada ya kutiliana saini  makubaliano ya uuzaji wa mafuta kwa kutumia kadi ya Aiter Money Tap Tap , Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Mafuta cha Puma Oysterbay.
Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani),wakati wa hafla fupi ya makubaliano ya uuzaji wa mafuta kwa kutumia kadi ya Aiter Money Tap Tap , Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Mafuta cha Puma Oysterbay jijini Dar es salaam. kushoto na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...