THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

KILIMANJARO QUEENS KULILETA KOMBE KESHO MCHANA.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jami.
MABINGWA wa Kombe la Chalenji la CECAFA, timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania Bara maarufu kwa jina la Kilimanjaro Queens, inatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam kesho Septemba 22, 2016 saa 7.00 mchana kwa ndege ya FastJet ikitokea Mwanza.

Mara baada ya kutua, itakwenda moja kwa moja kwenye Hoteli ya Coartyard iliyoko Sea View, Upanga jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata chakula cha mchana ambako watakuwako viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wale wa Serikali akiwamo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi.

Timu hiyo leo Septemba 21, 2016 ilitua Kagera ambako imetumia siku ya leo kuwafariji wahanga wa tetemeko la ardhi.

Itakumbukwa kwamba kabla ya kwenda Jinja, Uganda ambako ilivuna ubingwa huo katika fainali zilizofanyika jana kwa kuilaza Kenya katika fainali zilizofanyika Uwanja wa Njeru, Kilimanjaro Queens iliweka kambi mjini Bukoba ambako ilicheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Burundi na kushinda mabao 3-0 Septemba 8, mwaka kwenye Uwanja wa Kaitaba.

Kilimanjaro Queens imerudi Kagera kusema: “Ahsante” kwa wenyeji akiwamo Mkuu wa Mkoa, Brigedia Jenerali Mstafu Salum Kijuu aliyewakabidhi bendera kabla ya safari, lakini pia kuwapa pole Wahanga wa janga la Tetemeko la Ardhi wakazi lililotokea katika mikoa huo na mikoa jirani ya Kanda ya Ziwa na nchi jirani. Mikoa ambayo iliathirika zaidi ni Kagera na Mwanza kadhalika nchi jirani za Uganda na Rwanda.

Mara baada ya kuwapa pole, timu hiyo itasafiri kutoka Kagera kwa usafiri wa anga ambako taratibu za safari hiyo zitatangazwa na TFF hapo kesho ambako wananachi watapata fursa ya kuipokea na kuishangilia timu hiyo inayonolewa na Kocha Sebastina Nkoma akisaidiuwa na Edna Lema  wakiwa chini ya Mwenyekiti wa soka la wanawake, Amina Karuma.

Safari ya ubingwa wa Kilimanjaro Queens ulianzia hatua ya makundi kwa kuilaza Rwanda manbao 3-2 kabla ya kutoka sare tasa na Ethiopia ambayo pia ilivuna ushindi wa mabao 3-2 kutoka kwa Rwanda. Tanzania na Ethiopia zilitoka sare na kurusha sarafu ambako Tanzania ikawa ya kwanza katika kundi B hivyo kucheza na Uganda ambayo ililala kwa mabao 4-1 katika mchezo wa nusu fainali. Na leo Septemba 20, 2016 ikatawazwa kuwa mabingwa kwa ushindi wa mabao 2-1.