Tunapoadhimisha miaka mitatu ya kumbukumbu ya kifo cha Mtoto wetu mpendwa FLORA FLOWIN MKANULA (pichani), ni vyema kumshukuru Mungu hasa kwa mapendo aliyotushirikisha na kutuachia kupitia maisha yake FLORA.
Tunaadhimisha Misa Takatifu kesho tarehe 10/09/2016 saa 12.00 asubuhi katika kanisa la Mtakatifu Joseph Jijini Dar es Salaam.
Baada ya Misa tunazuru tulipomlaza mpendwa wetu Flora Mkanula Kinondoni kuyaenzi matendo yake mema.
Baada ya hapo tutaendelea kwa tafakari ya pamoja nyumbani kwa Wazazi wake Bw/Bibi F. Mkanula Yombo Vituka jijini Dar es salaam muda muafaka saa 7.00 mchana.
Raha ya milele umpe ee Bwana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...