Waigizaji wa Kundi la sanaa la Vitimbi toka nchini Kenya, wakizungumza mara baada ya kutoa moja maigizo yao katika Tamasha la 35 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, linaloendelea kufanyika kwenye Ukumbi wa Chuo cha Sanaa (TaSuBa), Bagamoyo Mkoani Pwani. Wakizungumza na waigizaji hao walisema kuwa wanafuraha sana kushiriki kwenye Tamasha hilo, kwani ni kubwa na la kuvutia sana, pia wametoa wito kwa Waigizaji wa Kitanzania kuungana na wale wa Kenya na kufanya kazi kwa pamoja kwani wanaamini wakiungana wanaweza kufanya kazi nzuri sana.
 Waigizaji wa Sanaa ya Vichekesho kutoka nchini Kenya, Mama Kayaii na Mama wa Mahakama, wakitoa burudani ya moja ya maigizo yao ya jukwaani kwa watazamaji waliojitokeza kwenye Tamasha la 35 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, linaloendelea kufanyika kwenye Ukumbi wa Chuo cha Sanaa (TaSuBa), Bagamoyo Mkoani Pwani.
 Waigizaji wa Kundi la Vitimbi kutoka nchini Kenya, Ondieki, Profesa na Sukuma Wiki wakiigiza jukwaani katika Tamasha la 35 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, linaloendelea kufanyika kwenye Ukumbi wa Chuo cha Sanaa (TaSuBa), Bagamoyo Mkoani Pwani.
Igizo likiendelea.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamadini Bagamoyo (TaSuBa), Dkt. Herbert Makoye (kushoto) akizungumza na baadhi ya Waigizaji wa Kundi la sanaa la Vitimbi toka nchini Kenya, mara baada ya kutoa burudani ya kuvutia kwa WanaBagamoyo, waliofurika kwa wingi kwenye Ukumbi wa Chuo cha Sanaa (TaSuBa), Bagamoyo Mkoani Pwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...