Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma

Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inaendelea kukutana na wadau tofauti wanaohusika na masuala ya uchumi katika kuhakikisha uchumi wa nchi unaendelea kukua.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe mijini Dodoma aliyetaka kujua hali ya uchumi ilivyo kwa sasa hapa nchini.

Waziri Mkuu amesema kuwa lengo kuu la Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha uchumi wa nchi unaongezeka kupitia nyanja tofauti kwa kushirikiana na taasisi za fedha zilizopo ili kufikia uchumi wa kati kama ilivyoanishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi Akizungumza kuhusu suala la midororo wa upokeaji wa mizigo katika bandari nchini, Waziri Mkuu amesema kuwa mdororo huo umetokana na kupungua kwa kiasi cha mizigo na kushuka kwa uchumi duniani.

Katika suala ya mauaji yaliyotokea Tanga, Mwanza na Vikindu, Waziri Mkuu amesema kuwa usalama wa wananchi utaendelea kuimarishwa huku serikali ikiahidi kupambana vitendo vya mauaji kwa raia na askari katika maeneo mbali mbali nchini.

“Serikali imesikitika sana na jambo hili la mauaji hivyo itahakikisha wauaji hao wanawekwa katika mikono ya Sheria na kuongeza ulinzi kwa maeneo yote nchini kwa kuanzia ngazi ya vitongoji” alifafanua Waziri Mkuu.

Mbali na hayo Waziri Majaliwa ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya dola katika kuthibiti matukio hayo.

Kuhusu suala la uwepo wa tozo katika zao la korosho swali limeibuliwa na Mbunge wa viti maalumu Mhe.Riziki Lulida (CUF), Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa Serikali imeshatoa maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kusimamia uondoaji wa Tozo zisizo na maana katika zao la korosho.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akisalimiana na Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzania Bungeni na Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe (MB) wakati wa kikao cha tatu cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzania na Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe (MB) akimuuliza swali Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) kuhusu hali ya uchumi nchini ambapo Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa alimhakikishia kuwa Serikali ipo imara katika kusimamia ipasavyo uchumi wa nchi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akijibu maswali ya wabunge wakati wa kikao cha tatu cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akiwashukuru wabunge mara baada ya kumaliza kujibu maswali wakati wa kikao cha tatu cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Leo Mjini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...