Mwenyekiti wa soka la wanawake Amina Kaluma akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na semina elekezi kwa timu za wanawake zinazotarajia kushiriki ligi kuu ya wanawake itakayotimua vumbi hivi karibuni, (Kulia) Ofisa habari wa Shiriksho la Mpira wa Miguu TFF Alfred Lucas na Makamu Mwenyekiti wa Soka la wanawake Rose Kisiwa (Kushoto) 


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeandaa semina elekezi kwa klabu za Ligi Kuu za wanawake inayotarajiwa kuanza baadaye mwaka huu.

Semina hiyo kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo, itafanyika Jumamosi Septemba 3 mwaka huu ikiwa ni kwa ajili ya kuwapa maelekezo mbalimbali na kanuni.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake , Amina Kaluma pichani kushoto,amesema kuwa hii ni moja ga fursa itakayosongesha mbele soka la wanawake nchini.

Kaluma amesema kuwa makocha wote pamoja benchi la ufundi watapewa semina elekezi kuhusu kanuni za ligi, usajili wa timu na taratibu nyingine za ligi hiyo ikiwa ni pamoja na sheria za mpira wa miguu ambazo zimekuwa na marekebisho kwa msimu wa 2016/2017 kama zilivyotolewa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Kaluma amesema ligi hiyo itaanza kwa mfumo wa makundi mawili ambao katika kila kundi zitatoka timu tatu zitakazocheza na kupatikana kwa mshindi wa kwanza, pili na tatu.

Timu zitakazoanza kushiriki ligi mwaka huu ni Viva Queens ya Mtwara, Fair Play FC ya Tanga, Panama FC ya Iringa, Mlandizi Queens ya Pwani, Marsh Academy ya Mwanza, Baobao Queens ya Dodoma, Majengo Queens ya Singida, Kigoma Sisters FC ya Kigoma, Kagera Queen pamoja na JKT Queens, Mburahati Queens na Evergreen Queens za Dar s Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...