KITUO cha Redio cha Magic FM  cha jijini Dar es Salaam wamepewa onyo kali na kumwomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKT.John Pombe Magufuli, wasikilizaji na wanaanchi kwa ujumla kwa kosa la kukiuka kanuni za huduma za utangazaji (Maudhui) za 2005.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA),  Bw. Joseph Mapunda 
amesema kuwa Magic FM wanatakiwa kuomba radhi kwa siku tatu mfululizo katika taarifa za habari za kuanzia saa kumi alasiri hadi saa tatu usiku kuanzia Septemba 17-19 mwaka huu.
Kwa upande wa Kituo cha utangazaji cha Redio 5 cha jijini Dar es Salaam kimepigwa faini ya shilingi milioni tano kwa kosa la kukiuka kanuni za huduma za utangazaji (Maudhui) za 2005 kupitia kipindi chake cha Matukio kilichorushwa hewani kati ya saa mbili na saa tatu usiku.

Pia kituo hicho cha Redio 5 kimefungiwa kwa miezi tatu kuanzia leo na vile vile kituo hicho kimewekwa chini ya uangalizi maalumu kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kipindi cha Kufungiwa Kumalizika.
Amesema kuwa haki ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo iko wazi ndani ya siku 30 kuanzia leo.
Uamuzi wa Kamati ya Maudhui Kuhusu lalamiko la ukiukaji wa Kanuni za huduma za Utangazaji (Maudhui), 2005 wawakilishi wa vituo vyaMagic FM na Radio 5 jijini Dar es Salaam leo.







Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA), Joseph Mapunda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kutoa hukumu ya Vituo vya Redio  vilivyukuwa vimefungiwa  jijini Dar Salaam leo.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA), Joseph Mapunda akiwakabidhi  wamiliki wa vituo hivyo hati za hukumu.Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...