THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MASAUNI AWAONGOZA WAJUMBE WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI KUTOA MISAADA KITUO CHA WATOTO YATIMA MJINI GEITA.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimkabidhi fedha taslimu Shilingi 1,119,000, Msimamizi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Moyo wa Huruma kilichopo mjini Geita, Sista Adalbera Mukure kwa ajili ya kusaidia majukumu mbalimbali ya ulezi wa watoto hao. Fedha hizo zilitolewa na Masauni pamoja na Wajumbe wa Baraza hilo kwa lengo la kusaidia kituo hicho. Pia Baraza hilo lilitoa mchele gunia moja, kilo 50 za sukari, dumu la mafupta ya kupikia, sabuni Katoni 11 pamoja na fulana 100.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (aliyembeba mtoto) na Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga (kulia) wakiwa na baadhi ya watoto Yatima wa Kituo cha Moyo wa Huruma cha mjini Geita, mara baada ya Masauni kukabidhi fedha taslimu shilingi 1,119,000 pamoja na vyakula kwa kituo hicho ambapo misaada hiyo ilitolewa na Baraza la Usalama barabarani ambalo linaadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama mjini humo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (aliyembeba mtoto), Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga (kulia kwa Masauni),  pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani wakiwa katika picha ya pamoja na Watoto Yatima wa Kituo cha Moyo wa Huruma cha mjini Geita, wakati Mwenyekiti huyo wa Baraza pamoja na wajumbe wake kukitembelea kituo hicho na kukabidhi misaada mbalimbali. Tukio hilo lilifanyika mara baada ya Masauni kuizindua Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo inaadhimishwa Kitaifa mjini Geita. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.