THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

mashindano ya Airtel Rising Stars Taifa yaanza kutimua vumbi

Pazia la michuano Taifa ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars jana lilifunguliwa katika uwanja wa Kukumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam ambapo timu ya wavulana ya Temeke ilitoa onyo kali kwa timu shiriki kwa kuifunga Kinondoni 4-1.
Mchezo huo ulitanguliwa na mechi ya wasichana kati ya Arusha na Lindi ambapo Arusha waliibuka na ushindi wa 2-0. Magoli ya Arusha yalifungwa na Eva Michael dakika ya 39 kwa njia ya penati na pili likifungwa na Warda Alfonce dakika ya 60.
Katika mchezo wa Temeke na Kinondoni, Temeke walianza kwa kasi ya aina yake na kupeleka mashambuliazi ya mara kwa mara langoni mwa Kinondoni huku Kinondoni wakionekana kuzidiwa katika kila idara.
Temeke waliandika bao la kwanza kupitia kwa Ramadhan Kawambwa kaika dakika ya 14, kwa njia ya penati baada ya mchezaji wa Temeke kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari. Goli hilo lilipokelewa kwa shangwa na mashabiki wa Temeke.
Temeke awalipata bao lao la pili kupitia kwa Abirahi Uihuro mnamo dakika ya 34 ambaye aligongeana mpira kwa uzuri na Ismail Kovu na kisha kumchambua kipa wa Kinondoni kwa umaridadi wa hali ya juu na kuukwamisha mpira huo kimiani.
Mohammed Mbegu aliifungia Temeke bao la tatu katika dakika ya 40 na kuzidi kuzamisha jahazi la Kinondoni ambao walinekana kama vile wamesimama wakati mchezo ukiendelea.
Rosea Mpoma aliwaliza kwa mara nyingine tena Arusha baada ya kuifungia Temeke bao la tano katika dakika ya 53 baada ya kuachia shuti kali na kuzama moja kwa moja wavuni.
Alikuwa ni Abirahi Uihuro tena, ambaye aliiandikia Temeka bao la nne mnamo dakika ya 28 ya kipindi cha pili baada ya kuunganisha krosi iliyochongwa na Mohammed Mbegu kutoka upande wa kushoto mwa uwanja na kuendeleza karamu ya magoli kwa Temeke.
Kinondoni walipata goli ya kufuta machozi mnamo dakika 36, likifungwa na Shaban Mangula baada ya mabeki ya Temeke kushindwa kuokoa mpira wa kona.
Michuano hiyo ya Airtel Rising Stars itaendelea kesho kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam na kufikia tamati Jumapili, Septemba 11.

 Mshambuliaji wa Arusha, Jenifa Veina (kulia) akijaribu kufunga huku kipa wa Lindi akijaribu kuzuiya katika mashindano ya vijana ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam jana.
 Mchezaji wa Arusha, Diana Mosses (kulia) akiwania mpira na beki wa Lindi , Neema Hashim katika mashindano ya vijana ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
 Kiungo wa timu ya Arusha,Joyce Faraja (kulia) akiwatoka wachezaji wa Lindi katika mashindano ya vijana ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam
 
Kiungo wa timu ya Arusha,Joyce Faraja (jezi namab 13) akiwatoka wachezaji wa Lindi katika mashindano ya vijana ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam