THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Mashine ya MRI Yaanza Kazi, Uongozi Muhimbili Wapongezwa

Na John Stephen, MNH

Dar es Salaam, Tanzania. Mashine ya MRI katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepona baada ya kuharibiika tarehe 24/08/2016. Mashine hiyo iliharibiika baada ya kutokea hitilafu ya umeme. Tangu mashine hiyo imepona tayari wagonjwa 52 wamepatiwa kipimo cha MRI. 

Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare amesema baada ya mashine hiyo kuharibiika, mafundi wa Philips kwa kushirikiana na mafundi wa Muhimbili walibadilisha betri zote 31 na kufunga mpya ili kuongeza ufanisi katika mashine hiyo.
“Tarehe 26/08/2016, mafundi walibadilisha betri zote 31 na kufunga mpya ili kuongeza ufanisi katika mashine hii kwa kuwa betri za awali zilikuwa zimefungwa muda mrefu. Tarehe 28/08/2016 mafundi walibaini kwamba kifaa cha Gradient Module kilikuwa kimeharibiika na tayari hospitali kwa kushirikiana na Philips wameagiza kifaa hicho kutoka Uholanzi,” amesema Dk Lwakatare. 

Mmoja wa ndugu wa wagonjwa, Lazaro James, mkazi wa Singida amesema kwamba tangu kuharibiika kwa mashine ya MRI alikuwa akiisubiri na kwamba amefurahi baada ya kurejea kwa huduma hiyo. “Tunashukuru huduma za MRI zimerejea hapa Muhimbili, gharama zake ni nafuu kuliko kuliko kupata matibabu nje. Jambo lingine napenda kuwapongeza madaktari na wauguzi kwa utendaji bora. 


Naye Hawa Hussein mkazi wa jijini Dar es Salaam, ameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuwa imekuwa ikitoa huduma bora kwa wagonjwa. Hawa ameuopongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa kufanya juhudi za kuiwezesha mashine hiyo kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa. Amesema kwamba madaktari wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii hivyo wana imani wataendelea kupata huduma bora na kwa wakati.

Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa wakati Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akieleza jambo kwa waandishi wa habari leo. 
Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali hiyo akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya mashine ya MRI kuanza kufanya kazi. Kutoka kulia ni Mtaalamu wa MRI (MRI Technologist), Joshua Job na Daktari Bingwa wa Mionzi, Mussa Ndukeki wa hospitali hiyo. 
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano uliofanyika leo kwenye hospitali hiyo. 
Mtaalamu wa MRI (MRI Technologist), Medadi Mallaya akimuhudumia mgonjwa leo.


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    HAHAHAHAHA MAJI KUPWA NA MAJI KUJAA.............TIA MAJI TIA MAJI.