THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Mbunge Bonnah Kaluwa Achangisha Milioni 13.7 Ujenzi Kituo cha Yatima.

 Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa akinadi vitu mbalimbali katika harambee hiyo kuchangisha fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Tegeta, harambee iliyoendeshwa na Kanisa la Deliverance Centre Victorius (CVC), chini ya Mchungaji Jehu Mkono. Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa akizungumza katika harambee hiyo kuchangisha fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Tegeta, harambee iliyoendeshwa na Kanisa la Deliverance Centre Victorius (CVC), chini ya Mchungaji Jehu Mkono.

 MBUNGE wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa ameongoza harambee ya uchangishaji wa fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Tegeta, harambee iliyoendeshwa na Kanisa la Deliverance Centre Victorius (CVC), chini ya Mchungaji Jehu Mkono. Harambee hiyo ilifanyika katika Kanisa la Deliverance Centre Victorius Tegeta kwa Ndevu, jijini Dar es Salaam, ambapo Bonnah Kaluwa alikuwa mgeni rasmi na kufanikiwa kukusanya fedha shilingi 13,730,000 ambazo zilipatikana kwa michango ya waumini, wageni waalikwa na kufanyika kwa mnada ulionadi vitu anuai.

 Katika harambee hizo Mbunge, Kaluwa alitoa shilingi milioni mbili yeye pamoja na mumewe huku akiendesha mnada uliotunisha mfuko wa ujenzi wa kituo hicho. Awali akizungumza katika harambee hiyo Mwenyekiti wa umoja wa akinamama wa kanisa la CVC, Rose Haji Mwalimu alisema harambee hiyo itawezesha kupatikana kwa fedha za ujenzi wa kituo pamoja na upanuzi wa kanisa la CVC eneo la Tegeta mradi unaotarajia kutumia shilingi milioni 40.