Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji akifafanua zaidi kuhusu kampeni ya USIKATE TAMAA,jijini Dar leo .
 Mwanamuziki, Nurdin Bilal Ali maarufu kama Shetta akielezea safari yake ya muziki hadi kufika hatua aliyopo sasa, ambayo  binafsi amekiri kuwa kwake ni mafanikio makubwa. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji.
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji akizungumza kuhusu kampeni ya USIKATE TAMAA, Kushoto ni mwanamuziki Shetta na kulia na Kaimu Meneja Masoko wa Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Zainul Mzige.PICHA NA MICHUZI JR.

 kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) leo imefanya uzinduzi wa kampeni ambayo imepewa jina la USIKATE TAMAA ikiwa na lengo la kuhamasisha watu waliokata tamaa kuwa nao wana nafasi ya kufanikiwa.

Akizungumzia kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji alisema kuwa kampeni hiyo inalenga kuleta matumaini mapya katika jamii kwa watu ambao wamekuwa wakipoteza matumaini kutokana na hali ya ugumu wa kimaisha ambayo imekuwa ikiwakabili.

Alisema kampeni hiyo itakuwa ikitumia watu mbalimbali ambao wamefanikiwa na watakuwa wakitoa historia zao katika maeneo mbalimbali ambayo watatembelea, wakielezea jinsi walivyokuwa na maisha magumu hapo awali na sasa wamefanikiwa kimaisha.


“Kuna watu hawana uwezo na wanazungukwa na watu ambao wamekuwa wakiwaambia kuwa hawawezi kufanikiwa lakini kupitia kampeni ya USIKATE TAMAA wataweza kupata matumaini kutoka kwa watu ambao walipita katika maisha magumu na baadae wakafanya vyema,” alisema Fatema.

Mkurugenzi wa masoko huyo aliongeza kuwa kampuni ya MeTL pamoja na kufanya biashara lakini pia inaijali jamii na inapenda kuona watu wakifanikiwa kimaisha hivyo kupitia kampeni ya USIKATE TAMAA itaweza kusaidia watu wa aina mbalimbali waliopo katika jamii ya kitanzania wakipata matumaini mapya na kuongeza juhudi ili wafanikiwe.


“MeTL kupitia chapa yake ya MO inataka kuona watu wakiendelea kupambana na kufanikiwa, tunataka watu wafanikiwe na tuwape tuzo, tuwape sauti ya kusikika na huu ni mwanzo tu, kampeni hii itafanyika kwa muda mrefu zaidi,” alisema Fatema.

Kwa upande wa mwanamuziki, Nurdin Bilal Ali (Shetta) ambaye ametumika kama mmoja wa watu ambao wamefanikiwa, alielezea safari yake ya kimuziki na kusema kuwa awali alikuwa akiishi kwa moja ya wasanii wa muziki nchini na alikuwa akifanya kazi za nyumbani kwa mtu huyo lakini akiwa na nia ya kutafuta njia ya kutoka kimuziki na juhudi alizozionyesha zimemwezesha kuwa moja ya wasanii waliofanikiwa nchini.


“Unaweza kuwa unajiamini katika kipaji chako lakini bado watu wanakudharau, mimi nimewahi kuishi na mwanamuziki mkubwa nchini lakini najijua nina kipaji lakini kwakuwa nilikuwa natafuta njia ya kutoka kimuziki ilinibidi nifanye hivyo,“Ilikuwa naosha gari lake, naosha vyombo na hata kumwogesha mdogo wake lakini nilikuwa najua nini nafanya na nini nataka, msanii yule alikuwa anafahamiana na watu wengi na mimi ikanisaidia kupata njia ya kutokea na leo kwa hatua niliyofikia nimefanikiwa,” alisema Shetta.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hivi huwa ni mwiko kwa wanamziki wa bongo flava kukata nywele au kuchana nywela kawaida!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...