Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WATOA msaada wa kisheria wanaumuhimu katika kuwasadia wananchi kupata haki pale wanapokuwa na tatizo la kiseheria.
Hayo ameyasema leo Mkurugenzi wa Katiba na Ufatilliaji wa Haki wa Wizara ya Katiba na Sheria, Patience Ntwina,wakati wa utoaji wa mfano wa hundi kwa watoa msaada wa kisheria iliyotolewa na Mfuko Huduma za Kisheria (S.L.F)
Amesema kuwa wanaotoa msaada wa kisheria katika kufanya kazi kwa ufanisi. Ntiwina amesema kuwa kwa mfuko huo kutoa bilioni 19 kwa watoa msaada wa kisheria katika kutimiza miaka mitano wamesaidia wananchi katika kuweza kupata kazi.
Nae Mwenyekiti wa bodi ya mfuko huo na Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Joaquine De Mello amesema kuwa wakati wakifanya ziara magerezani wamekuta robo tatu ya walio magerezani ni watuhumiwa tu.
Amesema kuwa wanamuunga mkono , Mchungaji Kiongozi, Mama Getrude Lwakatare kwa kuwatolea dhamana watu hao na wengine wanatakiwa kwenda na kuanza kuuliza kwa katika vituo vya polisi .
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko huo, Scholastica Jullu amesema kuwa wanaotoa msaada wa kisheria wanaonekana watu wasio na thamani lakini ndio wamekuwa wakisaidia watu katika kupata haki.
Amesema kuwa kwa hali iliyofikia kunahitajika kuwepo kwa chombo cha serikali katika kuwaratibu wanaotoa msaada wa kisheria katika kufikia malengo ya ufanisi wa utoaji haki. Amesema wametoa billioni 20 kwa taasisi
 Mkurugenzi wa Katiba na Ufuatilliaji wa Haki wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Patience Ntwina akizungumza na watoa msaada wa kisheria leo jiji Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa Sheria (S.L.F)Jaji wa Mahakama Kuu Mhe.  Joaquine De Mello akizungumza na akizungumza na watoa msaada wa kisheria leo jiji Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Katiba na Ufatilliaji wa Haki wa Wizara ya Katiba na Sheria, Patience Ntwina akiwa katika picha ya pamoja na watoa msaada wa kisheria leo jiji Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...