THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MFUMUKO WA BEI UMEPUNGUA HADI ASILIAMIA 4.9.

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Epharaim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Mwenendo wa Bei za Bidhaa mbalimbali hapa nchini.

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Epharaim Kwesigabo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Epharaim Kwesigabo  kulia akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Kushoto ni Kaimu Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi hiyo Ruth Minja. Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa Mwezi Agasti 2016  umepungua hadi asilimia 4.9 kutoka asilimia 5.1 ya ilivyokuwa mwezi Julai.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo amesema kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma na huduma kwa mwaka ulioshia mwezi Agasti 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi julai 2016.

Amesema Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 103.28  mwezi Agasti 2015 na mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi mwezi Agasti 2015 umepungua hadi asilimia 7.0 kutoka asilimia 7.6  ilivyokuwa mwezi Julai mwezi 2016.

Kwesigabo amesema kupungua kwa mfumuko wa bei wa mwezi Agasti 2016 umechangiwa na kupungua kwa kasi ya bei za baadhi bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Agasti 2016 zikilinganishwa na bei za mwezi Agasti mwezi 2015.

Mwenendo wa wa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula ivinaonesha kupungua ni pamoja na bei ya samaki kwa asilimia 7.01 mafuta ya kupikia 7.02. na mbogamboga asilimia 6.9 

Amesema kuwa uwezo wa Shilingi 100 ya Tanzania kununua bidhaa na huduma umefikia sh. 96 na senti 92  ilivyokuwa mwezi julai 2016.

Mfumuko wa bei kwa nchi zingine za Afrika Mashariki, Kenya umepungua hadi asilimia 6.26  kutoka asilimia 6.39 mwezi Julai 2016, Uganda mfumuko wa bei umepungua hadi asilimia 4.3 kutoka asilimia 5.1 mwezi Julai,2016