MGODI wa Dhahabu wa Geita(GGM) ulifanikiwa kuchangia Shilingi Milioni  mia nne arobaini na nne (444,000,000.00) ambazo zilinunua madawati 6000 ambayo ni asilimia 25 ya michango iliyotolewa katika tukio la uchangiaji madawati mkoani Geita.

Akizungumzia mchango huo wa madawati,Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita  Terry Mulpeter amesema kuwa GGM inaendelea kujihusisha katika kuchangia elimu mkoani Geita kwa kuwa ndiyo fursa endelevu ya kuwakomboa wananchi na kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

“Kwa kutambua umuhimu wa elimu, GGM imekuwa ikitoa mchango mkubwa kwenye ujenzi wa miundo mbinu ya elimu, Mgodi umechangia zaidi ya Shilingi Bilioni 10 za kitanzania kujenga shule ya wasichana ya Nyankumbu Mkoani Geita ambapo zaidi ya wasichana 800 wanapata maarifa kwenye michepuo ya Sayansi” amesema Mulpeter.

Amesema kuwa mchango wa GGM umefanikisha pia shule hiyo kuwa na Kompyuta za pamoja na vifaa vya kisasa katika maabara  na mazingira ambayo ni rafiki kwa wanafunzi kujisomea pamoja na nyumba  bora kwa waalimu kuishi. 

Bw Mulpeter amesisitiza kuwa kuwa elimu ni mojawapo ya haki muhimu za binadamu.
“Elimu ni jambo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu, GGM inaamini kuwa kuweka mazingira bora ya kusomea ili watoto wetu wengi wahitimu vyema elimu ya msingi na sekondari na kuendelea na masomo ya juu  itakuwa chachu ya maendeleo la taifa letu” 

Mgodi wa GGM unaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini na kuahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika jitihada za kuleta wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...