Daraja la Makutopora linalounganisha Wilaya ya Chemba na Manyoni likiwa limekamilika kujengwa, daraja hilo limejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 628,247,000 na kisha kuzinduliwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru George Jackson Mbijima. Mbijima amewaasa wananchi wa wilaya zinazounganishwa na daraja hilo kutumia fursa ya uwepo wa barabara na miundombinu  mizuri katika kuboresha maendeleo yao.

mir2

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru George Jackson Mbijima akipita katika daraja la Makutopora linalounganisha Wilaya ya Chemba na Manyoni likiwa limekalika kujengwa, daraja hilo limejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 628,247,000 kutoka serikali kuu na kisha kuzinduliwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru George Jackson Mbijima.

mir3

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru George Jackson Mbijima akizungumza na wanafunzi na wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa madarasa mawili na matundu ya vyoo nane katika sekondari ya Chikuyu yenye thamani ya shilingi milioni 108, 448,49.

mir4

Afisa wa mradi akitoa maelezo  ya mradi wa ufuatiliaji naudhibiti wa mbu waenezao malaria, huku gharama ya mradi huo ikiwa ni shilingi milioni sita na nusu.

mir5

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru George Jackson Mbijima akizungumza na mamia  ya wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa kituo cha maarifa ya kupambana na ukimwi chenye thamani ya shilingi  87,584, 007. Mbijima amewaasa wakazi wa Manyoni kukitumia kituo hicho ili kiwasaidie katika mapambano dhidi ya Ukimwi.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...