Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba

Mkoa wa Shinyanga umekabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi na chakula vyenye thamani ya Sh. milioni 41,172 kwa uongozi wa mkoa wa Kagera ili kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkaoani humo hivi karibuni.

Makabidhiano hayo yalifanywa leo mjini Bukoba kati ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Telack ambaye aliambatana na baadhi ya viongozi wa mkoa na viongozi wa dini ambapo mkoa wa Kagera umewakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa huo Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu. 

Wananchi wa mkoa wa Shinyanga wameguswa na kadhia iliyopata wananchi wa Kagera, hivyo tukaamua kukusanya nguvu ya pamoja kama mkoa ili kuwafariji Watanzania wenzetu kutokana na matatizo waliyoyapata” alisema Bi Zainabu.

Mkuu huyo wa mkoa alifafanua mchango wa misaada waliyotoa kuwa ni paamoja na mabati ya geji 28 1400, saruji mifuko 750, mchele kilo 600, mahindi kilo 100 paamoja na nguo.

Bi. Zainabu aliongeza kuwa michango ya msaada huo imeunganishwa nguvu kutoka Serikali ya mkoa wa Shinyanga, taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali, sekta binafsi, masshirika ya dini, asasi za kiraia, wafanyabiashara, mogodi ya madini iliyopo mkoani humo na wadau wengine wa maendeleo.

Akitoa shukrani mara baada ya kupokea msaaada huo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Kijuu amewashukuru wananchi wa Shinyanga kwa kuwafariji, majitoleo yao kwana kuwajali katika kipindi hiki cha mpito cha athari za tetemeko lililoukumba mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu nguo kwa ajili ya waathirika wa Tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu akiongozana na mkuu wa Mkoa wa Shinyanga mara baada ya kupokea misaada kwa ajili ya waathirika wa Tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...