THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MKUU WA MKOA WA MTWARA,HALIMA DENDEGO ATOA WITO KWA WANANCHI KUPANDA MITI YA MIKOROSHO


Wakati serikali ikihamasisha jamii kutekeleza adhma yake ya upandaji wa miti, Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego amesema katika mkoa huo kila kaya inatakiwa kupanda miti 30 ya mikorosho kwaajili ya kutekeleza agizo la serikali sambamba na kukuza uchumi wa kaya.

Dendego aliyasema hayo wakati aliposhiriki zoezi la usafi na upandaji wa miti katika hospitali ya rufaa ya Ligula lililoandaliwa na waandishi wa habari wa mkoa huo kwa kushirikiana na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania.

Alisema mkoa huo kwa kiasi kikubwa uchumi wake unategemea zao la korosho hivyo katika kutekeleza agizo la serikali wananchi wa mkoa huo hawatapanda mti ni mti bali watatakiwa kupanda miti ya mikorosho ambayo pia itawasaidia kukuza uchumi wao kwa faida.

"Wazo la waandishi wa habari kufanya usafi na kupanda miti linapaswa kuigwa na watu wote, tunataka nchi yetu iwe nadhifu na serikali imetoa agizo la upandaji miti,sisi kwa mkoa wa Mtwara hatutapanda mti ni mti tumeamua kila kaya itapanda miti 30 ya mikorosho ambapo itasaidia kuinua uchumi wa kaya,mkoa na taifa kwa ujumla lakini pia tutakuwa tumetekeleza agizo la kiserikali la upandaji miti kwa hiyo miti tutakayopanda sisi itakuwa na faida zaidi,"alisema Dendego

Akizungumza Mkuu wa taasisi ya 'Vodacom Tanzania Foundation' Renatus Rwehikiza alisema kampuni hiyo imekuwa ikijihusisha na mambo mbalimbali ya maendeleo ya kijamii kupitia taasisi ya Vodacom Foundation kwa kuhamasisha na kutekeleza kwa kufadhili pale jamii inapohamasika.

Aidha alisema suala la usafi linalenga maeneo mbalimbali ili kuboresha mazingira na kuwa na afya bora kwa maendeleo ya taifa.

"Kampuni imekuwa ikijihusisha na mambo mbalimbali ya maendeleo ya kijamii kupitia taasisi yake ya misaada kwa jamii ya Vodacom Tanzania Foundation ambayo inagusa elimu, afya,kujikimu, na mazingira katika kutekeleza adhma ya afya kwa mazingira kwani tunahamasisha watu wakihamasika wanatekeleza kwa kuwafadhili, kwasababu usafi ni wa wote,kazini na pahala popote pa kazi ili kuwa na afya bora kwa maendeleo,"alisema Rweikiza

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mtwara Hassan Simba alisema zoezi la kufanya usafi na kupanda miti litakuwa likitekelezwa kila mwaka mwezi Septemba ikiwa ni moja ya njia ya kuhamasisha jamii juu ya upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira.

"Sisi tulianzisha huu utaratibu mwaka jana kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania na itakuwa ni zoezi endelevu kwasababu tunapaswa kuelimisha na kuhabarisha jamii, hivyo hatuna budi tukiwa kama wanahabari ni lazima tushiriki pia,alisema Simba.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Halima Dendego(wapili kushoto)akiambatana na Mkuu wa Vodacom Tanzania Foundation,Renatus Rwehikiza(kushoto) Meneja uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu(kushoto kwake)wakifanya usafi katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula, kwa kushirikiana na Chama cha waandishi wa habari cha mkoni humo sambamba na kupanda miti katika maeneo ya wazi ya hospitali hiyo,Zoezi hilo lilidhaminiwa na Vodacom Tanzania. 

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Halima Dendego(wapili kushoto aliepiga magoti)pamoja na Mkuu wa Vodacom Foundation,Renatus Rwehikiza wakimshuhudia Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Mtwara,Hassan Simba(kushoto)akimwagia maji mti uliopandwa na Mkuu wa Mkoa huo katika zoezi la kufanya usafi katika hospitali ya rufaa ya Mkoa huo, kwa kushirikiana na Chama cha waandishi wa habari cha mkoa huo sambamba na kupanda miti katika maeneo ya wazi ya hospitali hiyo.Zoezi hilo lilidhamiwa na Vodacom Tanzania.


Mdau wa habari mkoani Mtwara,Taabu Mtingita(kushoto)na Meneja uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu wakizoa taka wakati wa zoezi la kufanya usafi katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula, kwa kushirikiana na Chama cha waandishi wa habari cha mkoni humo sambamba na kupanda miti katika maeneo ya wazi ya hospitali hiyo.Zoezi hilo lilidhamiwa na Vodacom Tanzania.