THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MBWA DOMO BAYA MLINZI NAMBA ONE WA RAS MAKUNJA KAPOTEA, ANATAFUTWA KWA UDI NA UVUMBA

Huko  Ujerumani, hususan katika makao ya Kiongozi mkuu wa Ngoma Africa band nyumbani kwa Kamanda Ras Makunja hali imekuwa si shwari baada ya mbwa aina ya Bulldog mwenye jina la sajent Domo Baya (juu) mlinzi namba moja wa Ras Makunja ametioweka lindoni kwa muda wa siku tatu sasa na kikosi cha kuangalia wanyama cha mji wa Oldenburg kinamtafuta mbwa huyo mwenye umri wa miaka 14 ambaye mara nyingi ni mwenye vituko pale anapochoka kulinda.
Mmiliki wa mbwa huyo kamanda Ras Makunja amekaririwa  akimlalamikia mlinzi wake huyo kwa kudai kuwa "kama kachoka kazi atamfuta" Mwanamuziki huyo anamlalamikia Domo Baya kwa visa na kwamba siku hizi ana tabia za uzembe sana .
"Kishanigombanisha na jirani baada ya kuvamia swimming pool yao bila idhini ya wenyewe", anasema  Kamanda Ras Makunja wa Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni. Lakini wakati msako ukiendelea hebu sikiliza kazi zao at www.ngoma-africa.com
Kiongozi mkuu wa Ngoma Africa band Ras Makunja


Kuna Maoni 6 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Kamanada mlinzi kisha kuwa mzee sasa wakabidhi wanakutunziwa wanyama,enzi alikuwa tishio sasa mzee

 2. Anonymous Anasema:

  kamanda huyo mlinzi wako kishachoka kazi kwa umtimui utafute mwingine weh mlinzi gani hana nidhamu kazini

 3. Anonymous Anasema:

  DUH KWELI KAMANDA HATAKI MCHEZO MLINZI SURA IMEKASILIKA NAMNA HII

 4. Anonymous Anasema:

  kudadeki hii bulldog ikikuvamia maisha kwishneyi eh!

 5. Anonymous Anasema:

  Si Mchezo mbwa katoweka kwa mkuu wa Ngoma Afrika aka pia watoto wa mbwa
  Jibwa limeshakuwa zee hilo kamanda tafuteni mlinzi mwingine

 6. Anonymous Anasema:

  Kamanda hili dubwana jibwa si dudu zuri kuwa nalo home ni hatari kwa wageni