Huko  Ujerumani, hususan katika makao ya Kiongozi mkuu wa Ngoma Africa band nyumbani kwa Kamanda Ras Makunja hali imekuwa si shwari baada ya mbwa aina ya Bulldog mwenye jina la sajent Domo Baya (juu) mlinzi namba moja wa Ras Makunja ametioweka lindoni kwa muda wa siku tatu sasa na kikosi cha kuangalia wanyama cha mji wa Oldenburg kinamtafuta mbwa huyo mwenye umri wa miaka 14 ambaye mara nyingi ni mwenye vituko pale anapochoka kulinda.
Mmiliki wa mbwa huyo kamanda Ras Makunja amekaririwa  akimlalamikia mlinzi wake huyo kwa kudai kuwa "kama kachoka kazi atamfuta" Mwanamuziki huyo anamlalamikia Domo Baya kwa visa na kwamba siku hizi ana tabia za uzembe sana .
"Kishanigombanisha na jirani baada ya kuvamia swimming pool yao bila idhini ya wenyewe", anasema  Kamanda Ras Makunja wa Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni. Lakini wakati msako ukiendelea hebu sikiliza kazi zao at www.ngoma-africa.com
Kiongozi mkuu wa Ngoma Africa band Ras Makunja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kamanada mlinzi kisha kuwa mzee sasa wakabidhi wanakutunziwa wanyama,enzi alikuwa tishio sasa mzee

    ReplyDelete
  2. kamanda huyo mlinzi wako kishachoka kazi kwa umtimui utafute mwingine weh mlinzi gani hana nidhamu kazini

    ReplyDelete
  3. DUH KWELI KAMANDA HATAKI MCHEZO MLINZI SURA IMEKASILIKA NAMNA HII

    ReplyDelete
  4. kudadeki hii bulldog ikikuvamia maisha kwishneyi eh!

    ReplyDelete
  5. Si Mchezo mbwa katoweka kwa mkuu wa Ngoma Afrika aka pia watoto wa mbwa
    Jibwa limeshakuwa zee hilo kamanda tafuteni mlinzi mwingine

    ReplyDelete
  6. Kamanda hili dubwana jibwa si dudu zuri kuwa nalo home ni hatari kwa wageni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...