THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MOROGORO KUANDAA KONGAMANO LA UWEKEZAJI KUTANGAZA FURSA ZILIZOPO MKOANI HUMO.

 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven Kebwe akizungumza na waandishi wa habari katika Mkutano uliofanyika kwenye Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Jijini Dar es salaam juu ya uwepo wa Kongamano la Uwekezaji litakalofanyika Mkoani Morogoro Septemba 29-10, 2016 lenye lengo la kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo Mkoani humo, kwani umejaaliwa kuwa na mazingira mazuni na uwepo wa rasilimali nyingi ambazo bado hazitumika ipasavyo, pia amewataka vijana wa kitanzania kuacha kukimbilia mijini na badala yake wajikite kwenye fursa ya uwekezaji wa kilimo na ufugaji. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford Tandari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford Tandari akifafanua jambo katika Mkutano huo na Waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam juu ya uwepo wa Kongamano la Uwekezaji Mkoani Morogoro litakalofanyika Septemba 29-10, 2016 , ambapo amesema kuwa Kongamano hilo litasaidia kuutangaza Mkoa wa Morogoro kama miongoni mwa maeneo yenye fursa na mazingira mazuri ya kibiashara kwa Makampuni ya ndani na nje ya nchi.
Mkutano huo ukiendelea.